skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Kamanda wa jeshi la polisi jijini Mwanza SACP Ramadhani Ng’anzi amesema jeshi la polisi mkoani humo limefanikiwa kupokea jumla ya silaha tano zilizosalimishwa na wananchi kufuatia zoezi la kusalimisha silaha katika vituo vya polisi,ofisi za watendaji pamoja na ofisi nyingine za serikali.

Kamanda Ng’anzi amesema kuwa wilaya ambazo wananchi wamesalimisha silaha ni pamoja na wilaya ya Ilemela ambapo kulikuwa na silaha tatu,  Bastola moja  na Shortgun mbili na wilaya ya Magu kulikuwa na silaha aina ya Shortgun na wilaya ya Sengerema  kulikuwa na silaha aina ya Gobole.

“Kuanzia leo tar 01/12/2021 tumejipanga na kuunda kikosi maalum ambacho kitapita nyumba kwa nyumba,mtaa kwa mtaa,wilaya na wilaya kuzisaka silaha zote ambazo zinazmilikiwa kinyume na sheria”Amsema Ng’anzi

Amesisitiza kuwa Jeshi la polisi jijini Mwanza limewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi ambao si waaminifu.

Kwa mujibu wa sheria ya kudhibiti silaha na risasi sura 223, serikali imetoa tangazo namba 774 la tarehe 29/10/2021 kama Notisi ya Msamaha wa kutoshitakiwa Kwa Watu Wanaomiliki Silaha kinyume na sheria ikiwa watasalimisha silaha hizo katika kipindi cha kuanzia tarehe 1 Novemba, 2021 mpaka tarehe 30 Novemba, 2021.

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa ambayo baadhi ya wakazi wake wanamiliki na kutumia silaha kiyume na sheria na kumekuwepo na matukio mbalimbali ya utekaji na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Imeaandaliwa na Matinde Nestory

Mhariri: Adela Madyane

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma