skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Kila mwaka ifikapo tarehe 20 Juni, dunia huadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, siku ya kimataifa ya kuwaenzi watu ambao wamelazimika kukimbia nchi zao na kuomba hifadhi nchi za jirani.

Siku ya Wakimbizi Duniani ni siku ya kimataifa iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwaenzi wakimbizi kote duniani. Huangukia kila mwaka tarehe 20 Juni na huadhimisha nguvu na ujasiri wa watu ambao wamelazimika kukimbia nchi yao ili kuepuka migogoro au mateso.

Wakimbizi Zaidi ya 200000 wanaohifadhiwa katika kambi za magharibi mwa Tanzania ni miongoni mwa mamilioni ya wakimbizi duniani ambao wanasherehehea siku hii kwa hisia tofauti wengi wakihoji ni linin chi zao zitatengemaa kiusalama na kisiasa ili warejee nyumbani.

Mkimbizi wa Burundi anayeishi katika kambi ya Nduta anayedai kuwa hadi ssa Burundi hakuna usalama wa Uhakika

Maadhisho ya mwaka huu yanafanyika nchini Tanzania katika Kambi ya Nyarugusu yenye wakimbizi mesto wa Burundi na DRC huku kukiwa na waomba hifadhi wapya zaidi ya elfu kumi kutoka mashariki mwa DRC wanaokimbia machafuko mapya na mapambano baian ya majeshi ya serikali na waasi wa M23

Siku ya Wakimbizi Duniani inaangazia haki, mahitaji na ndoto za wakimbizi, kusaidia kuhamasisha utashi wa kisiasa na rasilimali ili wakimbizi wasiweze kuishi tu bali pia kustawi. Ingawa ni muhimu kulinda na kuboresha maisha ya wakimbizi kila siku, siku za kimataifa kama vile Siku ya Wakimbizi Duniani husaidia kuangazia ulimwengu juu ya masaibu ya wale wanaokimbia migogoro au mateso. Shughuli nyingi zinazofanyika Siku ya Wakimbizi Duniani hutengeneza fursa za kusaidia wakimbizi.

Hata hivyo Wakimbizi nchini Tanzania wanapitia wakati mgumu kutokana na kupungua kwa misaada ya kiutu ikiwemo chakula ambacho mgao wake umepunguzwa kwa asilimia 50 hali inayoamsha malalamiko makubwa. Raia hawa kutoka Burundi na DRC ni wahanga wa Maisha magumu katika kambi za wakimbizi

Inaelezwa kuwa kupungua kwa misaada kutoka kwa wahisani kunatokana na ongezeko kubwa la wakimbizi duniani hususani vita vya Ukraine na Urusi, magigano ya Sudan sambamba na kushuka kwa viwango vya uchumi  duniani pamoja na babadiliko ya vipaumbele vya nchi wanaotoa mchango mkubwa kwa shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR

Kupungua kwa misaada kunaleta adha na changamoto ni nyingi katika Maisha ya wakimbizi nchini Tanzania hususani Chakula, huduma za afya, ukosefu wa nishati ya kupikia na vijana kukosa fursa za elimu ya juu kama ambavyo mwenyekiti wa jumuiya ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu Bw. Manilakiza Japhet wakati akiwasilisha maelezo ya wakimbizi kwa viongozi wa mashirika ya umoja wa mataifa aanabainisha kuwa tatizo ni kumbwa sana kuliko inavyotazamwa na jumuiya ya kimataifa huku akibainisha kuwa huduma za afya na elimu nazo ni changamoto

Kilio cha wakimbizi nchini Tanzania kimekuwa cha muda sasa hususani suala la kupungua kwa chakula na changamoto ya nishati ya kupikia, hali hii inaongeza machungu kwa wakimbizi hususani wanawake kwakuwa wao ndio wahanga wakuu wa matatizo yanayozikumba kaya zao hasa zinazogusa malezi ya Watoto. Hali hiyo inamwamsha Maria Kipangula ambaye ameishi kambini kwa Zaidi ya miaka 20, ambaye anataja kuwa wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa mavazi yakiwemo ya usafi kwa wanawake pamoja na vitendo vya rushwa kwa baadhi ya walimu katika shule za sekondari ndani ya kambi

Kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa huduma na hifadhi ya wakimbizi, nchi mwenyeji anao wajibu wa kuhakikisha kunakuwepo na mazingira wezeshi kwa wakimbizi kuwa salama na kutoa fursa kwa mashirika mbalimbali kutoa huduma, Sudi Mwakibasi ambaye ni mkurugenzi wa idara ya wakimbizi Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi ya Tanzania anabainisha kuwa suala la kuruhusu wakimbizi kujiajiri au kufanya biashara limezuiliwa kwakuwa linaenda kinyume cha sheria za wakimbizi na kwamba kurushusu biashara ni kuzorotesha juhudi za kurejeshwa wakimbizi ambao nchi zao zina amani hususani Burundi

Mwanzoni mwa mwezi huu, UNHCR iliongoza ujumbe wa mabalozi kutoka nchi sita za umoja wa ulaya ambao huchangia pakubwa misaada inayoolewa kwa wakimbizi na wenyeji wao. Wahisani hao walijionea mazuri na madhila ya ukimbizi na kuahidi kuweka mikakati ya kutatua changamoto za wakimbizi na wenyeji

Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania Mahoua Parums ametaja kuwa UNHCR kwa kushirikiana na serikali pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa mataifa hususani WFP, wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhisho la changamoto za chakula na mahitaji mengine kwa wakimbizi ili kuondoa au kupunguza mizozo bainia ya wakimbizi na wenyeji kwakuwa wengi wa wakimbizi hulazimika kuvunja sheria kwa Kwenda vijijini kutafuta mahitaji

Siku ya Wakimbizi Duniani ilifanyika duniani kwa mara ya kwanza tarehe 20 Juni 2001, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 ya Mkataba wa 1951 unaohusiana na Hadhi ya Wakimbizi. Hapo awali ilijulikana kama Siku ya Wakimbizi ya Afrika, kabla ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuiteua rasmi kuwa siku ya kimataifa mnamo Desemba 2000.

Kauli mbiu ya siku ya wakimbizi duniani mwaka huu ni “matumaini mbali na nyumbani” matumaini ya wakimbizi wengi  wanaoishi nchini Tanzania yamegawanyika katika makundi mbalimbali hususani matumaini ya kurejea katika nchi zao endapo kutakuwa na usalama wa uhakika na matumaini ya kupata hifadhi katika nchi ya tatu yaani kwenda kuishi katika nchi za Ulaya, marekani na Australia.

Mwandishi: Prosper Kwigize

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma