skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Bariadi

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu, Mohamed Ally ameishukuru serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule kongwe ya msingi Bariadi.

Ameyasema hayo akiwa kwenye mwendelezo wa maazimisho ya miaka 46 ya chama hicho ambapo amesema serikali imetoa na inaendelea kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwemo elimu, maji afya na miundombinu ya barabara hivyo ni wajibu wa kila moja kutunza miradi hiyo.

Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu Comrade Mohamed Ally (mwenye kofia) akiteta jambo na viongozi wengine wa CCM

Awali mwalimu mkuu wa shule hiyo Kulwa Mtebe amesema shule hiyo ni kongwe ina jumla ya wanafunzi 1439, na ujio wa fedha hizo umeiwezesha kupata madarasa mapya huku akiiomba serikali kuendelea kuipatia fedha kwani bado inayo madarasa mengini kongwe ya mwaka 1976.

Katika hatua nyingine viongozi na wanachama wa chama hicho wakiongozwa na katibu wamepanda zaidi ya miti 1000 ikiwa ishara ya utunzaji wa mazingira shuleni hapo.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma