skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Watu wenye mahitaji maalumu mkoani Mwanza wametakiwa kuhamasishana ili kujitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Aug 23 mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa sensa ya watu na makazi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi katika mkutano wa wadau ambao umefanyika kwa lengo la kuhamasisha sensa ya watu na makazi katika chuo Cha ualimu Butimba mkoani Mwanza na kusema kuwa sensa itasaidia serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi kulingana na idadi ya watu Na eneo husika pamoja na kupatia ufumbuzi wa mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Bi Makilagi amesema kuwa sensa ya watu na makazi itasaidia kupata taarifa ya kujua idadi ya wanaume na idadi ya wanawake,umri,hali ya ndoa(kidemographia),kujua taarifa za kijamii, uchumi, na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi ambazo zitawezesha serikali na wadau wengine kupanga maendeleo ya watu Katika sekta mbalimbali za Elimu,miundo mbinu,Afya, hali ya ajira na Taifa kwa ujumla.

“Itakapofika saa sita na dakika moja usiku wa kuamkia Aug 23 mwaka huu watu wote watakaokuwa wamelala ndani ya mipaka yetu ya nchi ya Tanzania wote tutawahesabu tunapeana taarifa rasmi ili wote mume tayari kwa sensa ambayo itafanyika maeneo yote” amesema DC Makilagi.

Wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na watuu wenye ulemavu wakifuatilia maelekezo ya Mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuhusu sensa ya watu na makazi mwaka 2022

Ameongeza kuwa sensa itasaidia kupata taarifa za maendeleo,kisiasa,uchumi, hali ya  kibiashara pamoja na serikali kuandaa bajet na kuleta mahitaji kwa wananchi.

Nae Mratibu wa sensa Luhinda Constantine amesema kuwa sensa ya watu na makazi ni ya sita kufanyika nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa sensa hiyo itahusisha makarani wa sensa ambao watatembea kaya zote nchini na kufanya mahojiano na Mkuu wa kaya ambao watawasaidia kupata takwimu sahihi ili kukamlisha zoezi hilo.

Kwa upande wake meya wa jiji la Mwanza Constantine Sima amesema kuwa sensa ni muhimu kwa jamii pia itasaidia serikali kufahamu namna ya kufanya maendeleo hususani kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu.

Baadhi ya washiriki Katika mkutano huo wamesema kuwa kila mmoja ana wajibu na haki ya kuhamasisha zoezi Zima la kujitokeza Katika kushiriki sensa.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma