skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam

Hayawi Hayawi, huwa. Ndoto ya Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) aliyokuwa akiililia kwa muda mrefu hatimaye imetimia baad aya kukutana na Dr. Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. 

Katika tukio hilo lililoibua matumaini makubwa kwa mtoto huyo, hakutanabahi kuwa aliye mbele yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, lakini baada ya kugundua alishikwa na hisia kali.

Mtoto Hamimu alishikwa na butwaa pale ambapo Rais Samia alipojitambulisha kwake huku akiinama chini bila kuamini.

Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Rais kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini humo.

Rais Samia alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake ya Kikazi Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu haraka baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila msaada wowote.

Mhe. Rais aligharamia matibabu ya mtoto huyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa muda wa miezi sita.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma