Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na. Mwandishi wetu – Tabora
Kwa muda mrefu mikoa ya magharibi mwa Tanzania ikiwemo Tabora, Katavi na Kigoma imekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya uhakika ya usafiri na usafirishaji kulikotokana na kutokuwepo na barabara za lami kutoka Dodoma na mikoa mingine.
kufuatia hali hiyo serikali imekuwa ikiweka mikakati mahususi ya kujenga barabara na miundombinu mingine ikiwemo Reli na bandali kwa ajili ya kuboresha mifumo ya mawasiliano, usafiri na usafirishaji ambapo kwa upande wa mkoa wa Tabora tayari barabara kuu ya lami kutoka Dar es Salaam imekamilika huku ujenzi ukiendelea katika barabara kuu ya Nyakanazi Kasulu, Katavi Uvinza, Uvinza Kaliua na Sikonge Mpanda.
Akizindua barabara ya lami kutoka Nyahua – Chaya mkoani Tabora yenye urefu wa kilomita 85, Rais Samia Suluhu Hassan amebainisha nia yake ya kuunganisha mikoa hiyo kwa barabara za lami kwa kuiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha inasimamia ipasavyo viwango vya ubora na kasi ya ujenzi wa miradi yote ya barabara inayoendelea na kuhakikisha masharti yaliyoainishwa katika mikataba na wakandarasi inazingatiwa.
Rais Samia amebainisha kuwa barabara hiyo ya Nyahua – Chaya ambayo ujenzi wake ulifadhilia na Mfuko wa maendeleo wa serikali ya Kuwait kwa gharama ya shilingi bilioni 123.9 itasaidia kuunganisha kanda mbalimbali za Tanzania pamoja na mikoa ya magharabi ikiwemo kuinganisha tanzania na nchi za maziwa makuu ikiwemo Burundi na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia mkoa wa Kigoma.

Hata hivyo, licha ya serikali kugharimia fedha za walipakodi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, kumekuwepo na tatizo la watanzania wenyewe kuharibu miundombinu ya barabara, madaraja na alama za barabarani jambo linaloitia serikali hasara kubwa, kuhatarisha maisha ya watu na vyombo vya usafiri.
Tabia hiyo inamwamsha Rais Samia amewataka wananchi kuepuka hujuma hizo zinazoitia serikali hasara kubwa ambayo hutoa gharama kubwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Rais Samia yuko mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi akifuatana na Naibu Mkurugenzi wa mfuko wa maendeleoo wa serikali ya Kuwait Bw. Waleed SH. Albahar, Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na mtendaji mkuu wa TANROADS mhandisi Rogatus Mativila.