Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika inaadhimisha miaka 30 tangu kuasisiwa huku kukiwa…
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salaam
Kabla ya kuzindua Kamati hiyo, Mhe. Rais Samia amesema Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ndio uso na lango la nchi yetu, wageni wakija au ukitoka nje ya nchi lazma utapita Wizarani hivyo ni lazima yafanyike maboresho makubwa ili kuhakikisha inakaa vizuri na kutoa taashwira nzuri ya nchi yetu.
Aidha, Mhe Rais amegusia falsafa ya R4, Maridhiano, Ustahimilivu, Maboresho na Kujenga upya nchi yetu pale inapobidi ndio maana Wizara ya Mambo ya Nje inatakiwa iyabebe na kuyasemea.
Mhe. Rais Samia ametolea mfano Mafanikio ya Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani ni kutokana na Falsasa hiyo ya R4 ambayo imeleta Taaswira nzuri kwa nchi yetu, Kisiasa, kiuchumi pamoja na Maendeleo ya Jamii.