Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka…
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri
Katika mabadiliko hayo madogo, mheshikiwa Rais memteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Aidha Dr. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.
Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.