skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu, Kasulu

Mbunge  wa Jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma Profesa Joyce Ndalichako ambaye pia ni Waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ametoa vifaa vya ujenzi kwa shule ya sekondari ya Kasulu inayomilikiwa na Jumuiya ya wazazi ya Chama cha mapinduzi.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano amevitoa mapema leo kama sehemu ya ahadi yake aliyoitoa kwa shule hiyo kufuatia kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidatoo cha sit ana kushika nafasi ya pili kimkoa.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mheshimiwa Ndalichako amesema kuwa, shule hiyo licha ya kukabiliwa na mazingira magumu hususani miundombinu, wametimiza wajibu waoo ipasavyo na hivyo kumshawishi kutoa msaada huo ambao utawezesha kukarabatiwa kwa ofisi kuu ya walimu.

“Nilifurahishwa sana na matokeo yenu, milionesha ushujaa mkubwa licha ya mazingira mnayofundishia kutokuwa Rafiki, na ahadi yangu nitaendelea kuwasaidia na leo ninatimiza ahadi yangu niliyoitoa kwenu, nimeleta vifaa vyote mlivoomba na ninawapa pesa za kulipa fundi” alisema Prof. Ndalichako Mbunge wa Kasulu mjini.

Profesa Ndalichako akifurahia jambo wakati Katibu wa wazazi wilaya ya Kasulu akitoa shukurani

Aidha Profesa Ndalichakoo ametoa kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya malipo ya fundi ambaye atafanya kazi ya kukarabati ofisi ya walimu

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Mwalimu Denis Joseph, amemshukuru Mbunge huyo kwa moyo wa kutekeleza ahadi huku akitaja bayana kuwa, viongozi wengi wamekuwa na desturi ya kuahidi bila kutekeleza,, huku akiweka bayana kuwa shule yake imejizatiti ipasavyo kuhakikisha wanafunzi wanafanya vema katika masomo na mitihani yao

Mwalimu Denis ametaja kuwa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2022 wanafunzi zaidii ya 50 katii ya 90 walipata daraja la kwanza huku Watoto wawili tu wakipata daraja la tatu, hakuna darala la nne wala sifuri

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Kasulu Bw. Nduhilubusa Mapigano ameishukuru ofisii ya mbunge na mbunge mwenyewe kwa kutambua changamoto zinazoikabiri shule hiyo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuisaidia hususani kwenye ukarabati wa majengo ili Watoto wasome katika mazingira mazuri

Bw. Mapigano amemshukuru profesa Ndalichako kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa chama na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za elimu wilayani Kasulu huku akitaja kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kumpa ushirikiano mbunge huyo.

Naye menyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Kasulu Bw. Mbelwa Abdallah ametumia fursa hiyo kumtaja Mbunge wa jimbo hilo profesa Ndalichako kama mbunge wa vitendo, na kwamba ahadi anazotoa anatekeleza na hivyo kukipa chama heshima mbele ya jamii

Prof Ndalichako akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM (w) Kasulu ndugu Mbelwa Abdallah

“Wewe ni Mbunge wa pekee katika mkoa wetu, ukiahidi unatekeleza, tunajivunia kuwa na wewe na tunakuahidii kwamba tutaendelea kukupa ushirikiano ili jimbo na wilaya ya Kasulu ipige hatua zaidii kimaendeleo.” Amesisitiza Bw. Mbelwa Abdallah mwenyekiti wa CCM wilaya.

Sikiliza Ripoti kamili ya BUHA FM kwa kubonyeza picha hapa chini

Viongozi mbalimbali wa jumuiya na hama cha mapinduzi wilaya ya Kasulu na kata ya Murubona walikuwa ni sehemu ya hafla hiyo, huku wengi wao wakimtaja Mbunge huyo kama fursa kwa maendeleo ya wilaya ya Kasulu kutokana na anavyoyagusa mahitaji ya walio wengi badala ya mtu mmoja mmoja.

Wakati huo huo profesa Joyce Ndalichako Mbunge ametumia hadhira ya shule ya sekondarii ya Wazazi Kasulu, kuwahimiza wananchi kote nchini kujitokeza kuhesabiwa katika shughuli ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agostii 23 mwaka huu, akitaja kuwa sensa ni msingi wa maendeleo.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma