skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini mkoani Kigoma Profesa Joyce Ndalichako, amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa jingo maalumu kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU) linalojengwa katika hospitali ya Mji wa Kasulu (Mlimani).

Profesa Ndalichako amebainisha kuwa, ujenzi huo unaendelea vizuri na kumtaka mganga mkuu wa hospitali hiyo kuendelea kumsimamia mkandarasi ili kuhakikisha kunakuwepo na ubora kadili ya ramani na fedha zilizotengwa.

Nimefurahi kwamba pesa zinapoletwa katika jimbo la Kasulu, shughuli zinaanza mara moja, na kukamilika kwa ujenzi wa jengo hili kutaokoa wagonjwa wengi na pia kupunguza usumbufu wa kuwasafirisha wagonjwa mahututi kwenda Bugando” alisema Profesa Ndalichako (mbunge) na Waziri wan chi osisi ya Waziri mkuu, Ajira, Vijana, na wenye ulemavu

Awali, akitoa taarifa ya ujenzo huo Mganga mkuu wa hospitali hiyo ya Mlimani Kasulu Dr. Winistone Japhet alieleza kuwa, ujenzi huo ukikamilika litakuwa ni mkombozi kwa idara ya afua kwani jingo hilo litasaidia kupokea na kutoa huduma maalumu kwa wagonjwa mahututi wapatao 10 kwa wakati mmoja.

Dr. Japhet alibainisha kuwa Ujenzi huo umetokana na serikali kutoa kiasi cha shilingi 250,000,000 kutoka katika mfuko wa UVIKO 19 na kwamba kutakuwa na vyumba 10 maalumu vya wagonjwa, vyumba vya madaktari, vyumba vya kuhifadhi dawa nae neo maalumu ya kupumzikia ndugu wa wagonjwa.

ulikuwa tunapata shida sana wanapokuja wagonjwa mahututi wanaohitaji huduma maalumu na za kibongwa, tulitoa huduma chache kutokana na kutokuwa nae neo maalumu pamja na vifaa, tulilazimika kila mgonjwa mahututi kumsafirisha kwenda Bugando Mwanza sasa, kupatikna kwa za UVIKO 18 kutawaokoa wagonjwa na pia kuepuka adha ya kuwasafirisha kwa zaidi ya kilomita 500 kwenda Mwanza” alisisitiza daktari Winistone Japhet mganga mkuu.

Wakati huo huo Profesa Joyce Ndalichako amewagawia simu janja wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 30 zenye thamani ya shilingi milioni 6 kwa ajili ya kuwasaidia kukusanya taarifa na kuzituma katika ngazi ya halmashauri na kuwarahisishia utendaji kazi wao

Simu hizo ambazo ni sehemu ya ufadhili wa shirika la kuhudumia Watoto ulimwenguni UNICEF zinatajwa kuwa chachu na nyenzo muhimu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao pia walikwisha kupatiwa baiskeli mahususi kwa ajili ya usafiri wawapo katika majukumu yao ya kutoa huduma za afya na ushauri kwa jamii katika maeneo yao.

Ninawashukuru sana wadau wote wa maendeleo katika wilaya ya Kasulu hususani jimbo langu la Kasulu mjini kwa namna wanavyochangia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya, nipelekeeni salaam za shukurani kwa UNICEF pamoja na mashirika yote ambayo yanaunga mkono juhudi za mama Samia katika kutoa huduma kwa wananchi” alisisitiza Mheshimiwa Profesa Ndalichako

Profesa Ndalichako amewahimiza watumishi wa afya, wahudumu wa ngazi ya jamii kutumia vifaa vinavyotolewa na serikali pamoja na wahisani kwa uangalifu ili view na tija kwa jamii na kamwe wasijifikirie wao tu bali jamii inayohitaji huduma kutoka kwao.

Amemtaka pia mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kasulu kuwasimamia vema wahudumu wote wa afya na kuongeza ushirikiano baina ya taasisi za umma na wananchi.

Halmahsuri ya mji wa Kasulu ni miongoni mwa halmashauri 8 za mkoa wa Kigoma, na Mji wa Kasulu ni mji wa pili kwa ukubwa ukitanguliwa na manspaa ya Kigoma Ujiji. Aidha Mji wa Kasulu ni miongoni mwa miji 13 mhimu inayokuwa kwa kasi na maarufu kibiashara nchini Tanzania

Uchumi wa mji wa Kasulu unatokana na biashara za mazao, biashara za viwandani, mali asili na bidhaa nyingi huuzwa katika mikoa ya Katavi, Tabora na chi Jirani za Burundi na DRC.

Kwa mujibu wa shirika la takwimu la taifa Kasulu mjini panakadiliwa kuwa na watu Zaidi ya laki 2 na na tangu kuasisiwa kwake hakukuwa na jingo maalumu la wagonjwa mahututi jambo lililopelekea wagonjwa mahututi kuchanganywa na wasio mahututi au kusafirishwa kwenda katika hospitali binafasi za ndani nan je ya mkoa wa Kigoma.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma