Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu uria Tanzania Profesa Elfasi Bisanda amepongeza uamuzi wa shiriki la OHIDE kuanzisha kituoo cha Radio chenye mlengoo wa kijamii wilayani Kasulu, na kuelezea matumaini yake kuwa jamii, serikali na wadau wa maendeleo wataitumia Radio hii kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali.

Pongezi hizo amezitoa mapema jana alipotembelea studio za BUHA FM mjini Kasulu na kuridhishwa na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kukamilisha mradio huo ambao pia ameutaja kuwa wa kipekee mkoani Kigoma kutokana na dira yake inayoweka bayana ukuaji wa elimu, haki za watoto pamoja na huduma kwa wakimbizi
Profesa Bisanda ambaye pia ameteuliwa hivii karibuni kuwa mwenyekiti wa Bodi ya shirika la maendeleo, utu na uwekezaji (OHIDE) ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Buha FM ili kuhakikisha inafikia malengo yake.
Profesa Bisanda ambaye alifuatana na maafisa kadhaa wa Chuo kikuu Huria alikuwa katika ziara maalumu kutembelea shirika la OHIDE na kushuhudia ujenzi wa kituo cha Radio cha Buha