skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini mkoani Kigoma Profesa Joyce Ndalichako ambaye pia ni Wazirii wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu kazi, ajira, Vijana na wenye ulemavu ameanzisha mashindano maalumu ya mpira wa miguu kwa ajili ya kuhamasisha michezo na kuhimiza Sensa ya watu na makazi

Akizindua mashindano hayo katika kijiji cha Nyansha mjini Kasulu ambayo yamepewa jina la Ndalichako Cup, Profesa Ndalichako ameweka bayana kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji, kuwaweka vijana pamoja na kuhimiza wananchi hususani vijana kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi.

Profesa Ndalichako (mbunge) amesisitiza kuwa vijana ni nguvu kazi ya taifa na kwamba michezo ni sehemu moja wapo ya kuwaweka pamoja huku akiwasisitiza kuwa na mshikamano, kujituma katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika harakatii zake za kuliinua taifa katika sekta mbalimbali kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Profesa Ndalichako na viongozi wengine wa Chama na serikali wakishuhudia mechi ya ufunguzi wa kombe la Ndalichako kati ya timu ya Nyansha na Murubona

Mashndano hayo yanahusisha timu 16 ikiwa ni timu moja kutoka kila kata katika kata 15 za jimbo la Kasulu mjini pamoja na timu ya Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Kasulu

Katika mechii ya uzinduzi timu ya kata ya Murubona ilitoka kidedea baada ya kuifunga timuu ya Nyasha magoli 8 dhidi ya 7 kupitia mikwaju ya penalt kufuatia kumalizika kwa dakika 90 wakiwa wamefungana sare ya bao 1 kwa 1

Mtanange wa pili umechezwa jana katika Uwanja wa Umoja mjini Kasulu kati ya timu ya Kumnyika na timu ya UVCCM ambapo Vijana wa chama waliifurusha timu ya Kumnyika mabao 3 kwa nunge na kuiondosha katika mashindano hayo ambayo yapo katika mfumo wa mtoano

Timu nyingine zinazoshiriki mashindano hayo ya Ndalichako Cup ni Kumsenga, Mwilamvya, Ruhita, Heru Juu, Msambara, Murufiti, Mwanga na Murusi

waasanii mbalimbali walitumbuiza katika tamasha hilo la Ndalichako cup huku wengi waoo wakimshukuruu Mbunge wao pamoja na Rais Samia kwa kujipambanua bayana katika kuwatetea na kuwahudumia wananchi.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atazawadiwa Kikombe na shilingi 500,000 (laki tano) na timu zote 16 zimepatiwa jezi na mpira kwa kila timu.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma