skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini kupitia Mfuko wa jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma amekabidhi madawati 730 kwa halmashauri ya Kasulu Mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akikabidhi madawati hayo kwa viongozi wa wilaya ya Kasulu katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu mapema jana, Mbunge wa jimbo hilo Prof. Joyce Ndalichako amefafanua kuwa madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 59, na ametumia fursa hiyo kumpogeza rais Dkt.Samia Suluh Hassan kwa kuonesha njia katika sekta ya Elimu.

Aidha Prof. Ndalichako amesisitiza kuendelea kutumia fedha ya jimbo kwa maendeleo ya wananchi kwa kuunga mkono utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ambazo zitakuwa na tija ya moja kwa moja kwa wananchi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu amemshukuru mbunge hiyo kwa msaada huo na kueleza kuwa uwepo wake kwenye jimbo hilo umesaidia pakubwa wilaya hiyo kupiga hatua.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Kasulu Mji Noel Hanura amemshukuru Prof. Ndalichako kwa kuwa mbunge Kiongozi ambaye pamoja na majukumu makubwa ya serikali aliyonayo amekuwa na utamaduni mzuri wa kukutana na wananchi na kutatua kero zao.

Mapema akitoa taarifa kwa Mbunge huyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Dollar Kusenge amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya Madawati kwa shule za msingi.

Kusenge ameweka bayana kuwa halmshauri ya Mji wa kasulu pamja na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuna upungufu wa madawati 22,500 na anatoa wito kwa wadauu mbalimbali na wananchi kuunga mkono juhudi zinaooneshwa na Mbunge wa jimbo hilo pamoja na serikali ya awamu ya sita.

Profesa Joyce Ndalichako ni miongoni mwa wabunge wachache wanaotekeleza ahadi kwa vitendo ikiwemo usimamizi mahili na ufuatiliaji yakini wa miradii yote inayotekelezwa katika jimbo lake.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma