skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb) leo Septemba 01, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada, Mhe. Pamela O’Donnel katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Waziri Ndalichako ameishukuru Serikali ya Canada kwa kufadhili Mradi wa maboresho ya vyuo vya ualimu maarufu (UTC) wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 30, ulioiwezesha Wizara kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Vyuo vinne vya Ualimu.

Profesa Joyce Ndalichako katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi. Pamela O’Donnel

Waziri Ndalichako amevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Ndala, Mpuguso Kitangali na Shinyanga ambapo ameongeza kuwa ujenzi na ukarabati huo umeongeza ubora, fursa kwa wanafunzi wengi kujiunga na mafunzo ya ualimu pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Balozi Pamela O’Donnel amemweleza Waziri Ndalichako kuwa Serikali ya Canada itaendelea kuisadia na kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata fursa za elimu bora.

Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako akimsindikiza mgeni wake Balozi wa Canada nchini Tanzania Bi. Pamela O’Donnel mapema leo baada ya mazungumzo yenye tiza kwa ustawi wa elimu nchini Tanzania

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma