skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka watendaji wake kushirikiana kwa pamoja ili wananchi wapate huduma kwa wakati

Waziri Ndalichako ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha kujadili kazi za Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika Septemba 6, 2023 katika jengo la OSHA jijini Dodoma.

Baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamojan na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani)  wakati wa kikao hicho.

Aidha Prof. Ndalichako ameongeza kuwa kila mtendaji anajukumu la kutekeleza maagizo ya viongozi kwa haraka ili kuiwezesha serikali kufikia malengo na kuleta tija kwa wananchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amemuhakikishia Waziri Ndalichako kuwa majukumu ya ofisi hiyo yatatekelezwa kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma akiongea kwa niaba ya Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  amebainisha kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu huyo mpya ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya wizara pamoja na taasisi zake.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma