skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Uboreshaji wa mazingira kwa wawekezaji wazawa wa makampuni ya uchimbaji na uuzaji wa vifaa vya kuchimbia Madini umesaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi hususani vijana katika maeneo yenye migodi ya madini mbalimbali nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa kampuni ya Rock Solutions Tanzania Limited Zacharia Nzuki wakati akizungumza Waandishi wa habari  jijini mwanza mapema leo.

Bw. Nzuki amebainisha kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau imesaidia kuboresha mazingira na kuwawezesha wazawa kupata ajira, sabamba na kukuza vipaji na kupunguza utegemezi katika familia.

Mkurugenzi wa kampuni ya Rock Solutions Tanzania Limited Zacharia Nzuki akizungumza Waandishi wa habari  jijini mwanza

Aidha kampuni ya Rock Solution imekili kuwa Serikali ya Tanzania imewasaidia wawekezaji wazawa kupata nguvu ya kusambaza vifaa vya uchimbaji kwenye migodi, tofauti na awali ambapo vifaa vimekuwa vikisambazwa na watu kutoka mataifa ya ulaya.

Kampuni hiyo inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya uchimbaji wa Madini imefanikiwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 50, na wana ofisi Mkoa wa Mwanza , Arusha na Dar es salaam pamoja na kufanya kazi na migodi ya Barick,Geita Gold Mining,Shant Mining pamoja Nyazaga kwa kumpeleka  vifaa vya uchimbaji Madini.

Bw. Fabian Mayenga Meneja wa kampuni ya Rock Solutions Tanzania Limited Tanzania

Sanjari na hayo wameanzisha ujenzi wa kiwanda Cha vifaa vya utafiti kwenye migodi hii itasaidia vijana takribani 200 kujipatia ajira hali ambavyo itapunguza vijana kujiingiza kwenye tabia hatarishi,kiwanda kitaongeza Pato la taifa pamoja na kiwanda hicho kitahudumia vifaa nchi za Zambia na Congo.

Sanjari na hayo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaboreshea mazingira rafiki hali ambayo imesaidia vijana kujipatia ajira mbalimbali Kutoka kwenye makampuni ya uchimbaji na uuzaji wa vifaa vya uchimbaji Madini.

Kwa upande wake meneja Mkuu wa kampuni Fabian Mayenga amesema kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kutoa huduma za kijamii pamoja na kupanua wigo wa ajira kwa wananchi.Akizungumzia changamoto amesema ushindani wa kibiashara, Covid 19 imeathiri biashara ambapo bidhaa zinachelewa kufika nchini zinachukua mpaka miezi 3, pamoja na bandari ya Tanga iboreshwe ili kupunguza msongamano kwenye bandari ya Dar es salaam hali ambayo itasaidia kupakuliwa kwa mizigo meli inapotia nanga.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma