skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Matinde Nestory, Mwanza

Wazazi na walezi mkoani mwanza  wameshauriwa kufatilia mienendo ya watoto wao katika ngazi ya familia ili kuhakikisha makuzi na tabia zinakuwa za kimaadili.

Kauli hiyo imetolewa leo na mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr Thomas Rutachunzibwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari wanaopiga Vita matumizi ya dawa za kulevya na uharifu Tanzania (OJADAT) katika maadhimisho yaliyofanyika jijini Mwanza ya kupinga Vita matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu katika ukumbi wa mganga Mkuu wa Mkoa hospital ya Mkoa ya sekoutoure iliyopo jijini Mwanza.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr Thomas Rutachunzibwa

Dr Rutachunzibwa amesema kuwa wazazi na familia kwa ujumla kuhakikisha watoto wao wanaenenda katika maadili mema hali ambayo itasaidia kupunguza idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya.

“Familia ndio msingi mkubwa wa kuhakikisha kwamba tunathibiti matumizi ya dawa za kulevya katika jamii Zetu tukiwalea vizuri watoto wetu ukawafatilia tutakuwa tumewaepusha na hili janga la dawa za kulevya”amesema Dr Rutachunzibwa.

Ameongeza kuwa dawa za kulevya zinaathiri akili na ubongo vinakuwa katika  hali ya tofauti hali inayopelekea mtumiaji wa dawa za kulevya kufanya kitu chochote bila ya aibu.

Akizungumzia madhara ya dawa za kulevya  amesema kupata maambukizi ya homa ya Ini,Figo,TB,B&C,Ukimwi na magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya majimaji na damu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama Cha Waandishi wa habari wa kupiga Vita matumizi ya dawa za kulevya na uharifu Tanzania (OJADAT) Edwin Soko amesema  maadhimisho hayo hufanyika kila ifikapo Juni 26 ambapo mwaka huu kwa Mkoa wa Mwanza  tumeadhimisha June 30 huku yakiwa na kauli mbiu tukabiliane na mwenendo wa dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii.

Ameongeza kuwa Waandishi wa habari wanapaswa kuelimisha jamii kwa kuandika habari zitakazofanya jamii isitumie dawa za kulevya ambazo zina athari katika jamii,kielimu pamoja na kiuchumi hali itakayopelekea kupungua kwa matumizi ya dawa hizo.

“Nasisitiza dawa za kulevya hazina afya kwa jamii, dawa za kulevya ni nguzo mbaya Sana za mmomonyoko wa maadili na mstakabali wa maisha na umoja katika familia kwani Kuna athari kubwa katika kutumia dawa hizo”amesema Soko.

Waandishi wa habari katika picha ya pamoja na viongozi wa OJADAT Bw. Edwin Soko (kulia) Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr. Rutachumbizwa (katikati) na Dr. Eunice Masango Mratibu wa afya ya akili mkoa wa Mwanza

Nae mratibu wa afya ya akili Mkoa Dr Eunice Masango amesema kuwa dawa za kulevya zinaweza kumpeleka mtumiaji kutokuwa sawa kisaikorojia kwa sababu ya matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo na kuwa na hisia potofu ambazo hupelekea jamii kuzorota kiutendaji na wengine kushindwa kumudu masomo pamoja na kuwepo kwa ongezeko la umaskini,uharifu na ubakaji.

Aidha ameongeza kuwa ushauri nasaha unatumika zaidi katika hatua mbalimbali za tiba,dawa mbalimbali zinazotumika kumpunguzia mtumiaji uteja na usugu pamoja na hospitali mbalimbali za afya ya akili na dawa za kulevya.

Hata hivyo ametaja mikakati iliyopo ni pamoja na kuanzisha kwa vituo vyaTiba ya methadone ikianza na Manispaa ya jiji la Dar es salaam,Mwanza, Dodoma, Arusha,Tanga,Mbeya na Zanzibar pamoja na kutungwa kwa Sheria mpya itakayoziba mianya yote iliyopo hivyo itasaidia udhibiti wa tatizo la dawa za kulevya.

Aidha wameitaka jamii kuhakikisha kutowatenga wathirika wa dawa za kulevya kwa kuwapa ushauri ambao utawasaidia kutoka katika janga la matumizi ya dawa za kulevya. 

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma