skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mkuu wa mko wa Kigoma, Thobias Andengenye leo amzeweka ziwe la msingi la ujenzi wa nyumba za watumishi wa kada ya afya katika Hospitali ya wilaya ya Kasulu ambazo zinajengwa kwa kutumia fedha za ndani ya halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya kuweza jiwe hilo, mkuu huyoo wa mkoa amesema nyumba hizo zitakuwa ni kichocheo cha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kivutio kwa watumishii kufanya kazi kwa weledii na utulivu

Nyumba hizo 5 ambazo zimejengwa na mkandarai jeshi la Magereza Kasulu zina thamani ya shilingi milioni 291 na zimekamilika kwa asilimia 99 na zitaanda kutumika hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye (mwenye shati nyeupe katikati) Kisoma maandishi kwenye jiwe la msingi

Mganga mkuu wa wilaya ya Kasulu Dkt Josephat Rwebangila katika taarifa yake kwa mkuu wa mkoa amebainisha kuwa kutokana na kukosekana kwa nyumba za makazi, watumishi wengi walikuwa wakiishi mjini umbali wa takribani kilomita 15 ambapo hhulazimika kulipa nauli kila siku kiasi cha sh 5000 kwenda na kurudi kazini huku huduma za dharula kwa wagonjwa zikitolewa kwa shida.

wakazi wa wilaya ya Kasulu wanaopata huduma katika hospitali hiyo wamesifu uamuzi wa kujenga nyumba hizo na kutaja kuwa huduma zitaboreka zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma akipanda mtii wa kumbukumbu na kuashiria uzinduzi wa upandaji miti mkoani Kigoma

Wakati huo huo mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amezindua zoezi la upandaji mitii katika mkoa wa Kigoma kwa kupanda mitii katika hospitali hiyo na kuagiza kila halmashauri kupanda miti isiyopungua milioni moja ili kunusuru mazingira.

Akitekeleza agizo la Makamu wa Rais Philpo Mpango, mkuu huyo wa mkoa ametoa witoo pia kwa kila kaya kupanda angali miti 4 ikiwemo ya vivuli na matunda kama sehemu ya uwekaji wa mipaka ya makazi au viwanja vyao

BUHA FM ITAKULETEA HABARI KWA KINA KATIKA MAKALA YAJAYO ENDELEA KUSOMA UKURASA WETU WA TOVUTII NA MITANDAO YETUU YA KIJAMII KWA ANUANI YA @buhatanzania na TWITTER @buhafm

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma