skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane-Kigoma  

Mashirika yasiyo ya Kiserikali mkoani Kigoma yameaswa kuboresha miundombinu ya ofisi zake ili kutengeza mazingira ya kupata  fursa ya kushirikiana na taasisi za kimataifa hususan mashirika ya umoja wa mataifa yaliyoungana kutekeleza miradi ya maendeleo mkoni humo.

Hayo yamebainishwa na Afisa kutoka ofisi ya mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini Tanzania Bw. Kanali Rankho, ambaye anaratibu mradi wa pamoja wa Kigoma Joint Program (KJP) wakati akitoa wasilisho lake katika mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma ulioyofanyika katika ukumbi wa kanisa la Anglikana mjini Kigoma ambao unahudhuriwa na mashirika zaidi ya 100 ya ndani na nje ya mkoa wa Kigoma.

Bw. Rankho amesema lazima mashirika hayo yawe na ofisi zinazotambulika na kuajiri wataalamu katika kila sekta, lakini pia yawe na matumizi rasmi ya mitandao ya kijamii hususan website, na yaanze kufanya kazi  katika eneo lenye weledi wake kwa kutumia pesa za ndani kabla ya kupata ufadhili.

Bw. Kanali Rankho, ambaye anaratibu mradi wa pamoja wa Kigoma Joint Program (KJP)

Ameongeza kuwa taarifa za mashirika hayo zipatikane kwa njia ya kidigitali na yatumie mawasiliano rasmi ya barua pepe ya shirika na sio ya mtu binafsi hali ambayo itaonesha ni kwa namna gani wameshajiwekeza na watakuwa katika nafasi nzuri ya kupata mashirika ya kimataifa na makubwa kifedha kushirikana nayo.

“Mashirika yatakayokidhi vigezo hivyo yataonyesha kwamba  yapo tayari kufanya kazi na milango ya kushirikiana na  mashirika mengine  yakimataifa na yenye uwezo mkubwa kifedha yatakuwa tayari kufanya makubaliano ya kushirikiana na hata  fursa za kushirikiana na Kigoma joint program zitapatikana na itakuwa rahisi kwetu kuwahamasisha wadau wengine kushirikiana nao ” Amesema Rankho.

Aidha amesema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka katika mashirika hayo kwamba mashirika ya pamoja ya umoja wa mataifa yamekuwa hayashirikiani nao katika utekelezaji wa miradi inayofanywa na umoja wa mashirika mkoani Kigoma jambo ambalo linaashiria kwamba hawapati taarifa sahihi za kuomba kushirikiana nao au hazikikidhi vigezo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma

Akitoa mfano amesema baadhi ya mashirika yamekuwa na mfanyakazi mmoja anyesiamama katika nyadifa zote za ukurugenzi, afisa mwajiri, muhasibu na mhudumu wa ofisi, na kwamba ofisi hizo hufungwa mpaka pale watakapopata ugeni, na kusisistiza kuwa ofisi kama hizo haziwezi kupata ushirikiano kutoka mashirika ya kimataifa kwakuwa yanakuwa yamepoteza vigezo vya kufanya kazi kulingana na sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Kwa upande wake Msafiri Nzunuri mratibu na naibu msijili  wa mashirika  mkoani Kigoma amesisitiiza kuwa ni muhimu asasi zikaruhusu kujifunza zaidi na kukubali mabadiliko ili kuwa wafanisi zaidi katika kazi zao.

Amesema ofisi ambazo hazijikiti katika kufanya miradi mbalimbali bila pesa kutoka kwa mfadhili kwa kisingizio cha kukosa miradi zinajweka katika nafasi mbaya ya kutoshirikiana na taasisi nyingine kwasababu watapooteza ufanisi wao kwani hawatakuwa na ripoti yoyote ya kazi wala taarifa za fedha hazitaonesha mtiririko wa majukumu jambo ambalo halina afya kwa mashirika ya aina hiyo na kwamba wanapaswa kubadilika.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma