WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua jengo la wagonjwa wa dharura kwenye hospitali ya wilaya ya…
Habari na Ananias J.Khalula
Waswahilii wana msemo usemao kuwa Ng’ombe wa maskini hazai na kwamba akizaa anazaa dume, msemo huu una maana mtambuka sana katika jamii za kiafrika, lakini kwa mama Sharifa Yusuf ambaye ni mjane mkazi wa Muleba mkoani Kagera, kilichomkuta ni tafsiri tosha ya msemo huo
Jumla ya Ng’ombe 22 wamekufa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa wakiwa malishoni na kusababisha hasara kubwa kwenye Familia ya Mama Sharifa Yusuf katika Kijiji cha Katanga Kata Magata Wilaya Muleba Mkoani Kagera
Maafa hayo ya ya mifugo yametokea mnamo tarehe 21 mwezi 11 mwaka huu,.

Mmiliki wa mifugo hao Bi. Sharifa anasema familia yake imepata pigo kwani ilkuwa inategemea mifugo hao kama kitega uchumi cha familia na jamii kwa ujumla.
Bovya hapo chini kusikiliza majonzi ya mfugaji Mjane
Mkuu wa wilaya Muleba,Toba Nguvila ametoa pole kwa familia ya wafugaji hao na kutaja kuwa mvua iliyonyesha imesababisha hasara makubwa kwenye maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo.

Aidha katika hatua nyingine ambayo iliwashangaza wakazi wengi wa wilaya ya Muleba mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku kutotumia nyama za ng’ombe hao, majumbani au kwenye bucha bila kibali cha dakitari wa mifugo. Deaturi kwa waafirika wengi, mfugo ukipigwa na radi huliwa bila hofu, na jambo hili limekuwa likitahadharishwa na wataalamu wa mifugo, hivyo marufuku ya DC ililenta minong’ono miongoni mwa wana Muleba
Ikumbukwe kuwa matukio haya ya ng’ombe kupigwa na radi yamekuwa yakitokeza mara kwa mara katika nyakati tofauti na Mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na ng’ombe wapatao 554,380 wanaofugwa ambapo ng’ombe wa asili ni 534,299 na ng’ombe wa maziwa ni 20,081.
Kwa upande wa Mkoa Kigoma,tukio linalofanana na hili limewahi kutokea mwaka 2019 NG’OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12 ,walikufa baada ya Kupigwa na radi katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko.