skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Matinde Nestory, Mwanza

Wananchi mkoani mwanza wameshauriwa kutembelea vivutio vya Maliasili na utalii vilivyopo ndani ya Mkoa wa Mwanza ambavyo ni Chachu ya kuongeza Pato la taifa.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel katika maandamano ya matembezi ya mshikamano ya Royal tour ambayo imezinduliwa katika viwanja vya Rocky city mall vilivyopo wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza.

Mhandisi Gabriel amesema wananchi wametakiwa kwenda kujionea vivutio ambavyo vinapatikana mkoani hapa Bismarck Rocky,Saa nane national Park,Kituo Cha Makumbusho bujora,Jiwe la kuondoa matatizo,utalii wa boti katika ziwa Victoria ambavyo vinaongeza Pato la taifa na uchumi kwa ujumla.

“Sisi katika royal tour yetu Mkoa wa Mwanza tumeanza kutembelea vivutio vyetu tuvijue,tuvitangaze na tujenge utamaduni wa kuwa tunatembelea Mara kwa Mara na kurithisha watoto wetu”amesema RC Gabriel.

Ameongeza kuwa Rais amefanya Jambo la kimapinduzi katika sekta ya utalii kwa kuingiza watalii wapya,pia ni kiongozi ambaye amefungua uchumi wa Tanzania katika sekta ya utalii.

 Wageni kutoka mataifa mbalimbali waliokuja Tanzania kujionea vivutio vya  Mali asili na utalii Tanzania

Kwa upande wake Mkuu wa Kanda Idara ya utalii ya wizara ya maliasili na utalii Daines Kunzugala amesema kupitia filamu ya Royal tour itafunguka soko la kitaifa na kimataifa ambapo sekta ya utalii inaongoza katika kuingiza Pato la taifa kwa 17%,na fedha za kigeni 25%,pia inatoa ajira 5000 moja kwa moja na ajira 1,000,000 zisizo moja kwa moja.

“Sekta ya utalii ina umuhimu katika uchumi wa kiutamaduni , uhifadhi wa Mila za zamani kwa kizazi Cha Sasa na kijacho pamoja na uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya uchumi wa mtu mmoja mmoja” amesema Kunzugala.

Nae  Mwakilishi wa wabunge Mkoa wa Mwanza Kasalali Mageni amesema Royal tour imefungua fursa za ajira kwa vijana,kukuza utalii wa Tanzania pamoja na soko la watalii wa ndani kukua kwa kutengenezea fursa za mtu moja mmoja.

Wakati huo huo Afisa Elimu Sekondary Manispaa ya Ilemela Sylvester Mrimi amesema Watanzania wamefahamu vivutio vinavyo patikana katika hifadhi zao na kujua fursa za kazi zinazopatikana huko.

Nae Mwenyekiti Shirikisho la Walimu Makada Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Jackson Kadutu amesema kupitia Royal tour wilaya za Mkoa wa Mwanza wametambulisha vivutio  vinavyopatikana mkoani hapa pamoja na filamu hiyo imefungua milango ya uchumi wa Tanzania.

Hata hivyo amewaomba watanzania kutembelea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi za taifa,mapori ya akiba,misitu iliyohifadhiwa pamoja Makumbusho ambavyo vinaongeza Pato la Taifa.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma