skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Joel Daud, Muleba Kagera

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Bw. Toba Nguvila ameliagiza Jeshi la Polisi Wilayani Muleba mkoani Kagera kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio la mauaji ya kikatili yaliyotekelezwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Swaibu Mswadiku anayedaiwa kumuua mke wake kwa kumkatakata mapanga mauaji yaliyotokea Kata ya Magata Karutanga Kijiji cha Kasheno eneo la Kaina wilayani Muleba.

Maagizo hayo ameyatoa mara baada ya kufika eneo la tukio kijijini hapo na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo Bw.Nguvila mbali na kutoa maagizo kwa Jeshi la Polisi wilayani humo amewaelekeza Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Dini wakiwemo Viongozi wa Kimila wa eneo hilo kukutana mara moja ili kujadili suala la amani na usalama wa wananchi katika Kata ya Magata Karutanga wilayani Muleba.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imesema kuwa Mwanamke aliyeuliwa ni Bi. Zaidia Swaibu mwenye umri wa miaka 35 ameuawa kwa kukatwa na panga na anayedaiwa kuhusika na tukio hilo ni mume wake Bw.Swaibu Mswadiko mwenye umri wa miaka 48 ambaye mpaka sasa hajulikani alipo mara baada ya kutekeleza tukio hilo.

“Huyu aliyefanya kitendo hiki ni lazima sheria za nchi zichukuliwe dhidi yake, kuua ni kosa la jinai hatuwezi kumuacha ni lazima atafutwe popote alipo hivyo naagiza Jeshi la Polisi kumtafuta mtuhumiwa na akipatikana utaratibu wa sheria na kanuni kwa mujibu wa Katiba yetu uchukue mkondo wake” alisema DC Nguvila.

Pia,DC Nguvila amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka husika ikiwemo Jeshi la Polisi kufanikisha kupatikana kwa mtuhumiwa huyo wa mauaji ili akamatwe haraka na hatua kali za kisheria zichukuliwa dhidi yake.

“Mimi Mkuu wa Wilaya na Kamati yangu ya Usalama kitendo hiki kimetufedheesha sana, sihitaji kuona tukio jingine kama hili likifanyika tena na aliyefanya hiki kitendo atakapoonekana popote pale toeni taarifa haraka ili akamatwe”.Alisema

Naye Diwani wa kata ya Magata Karutanga Bw.Alhaji Yakubu Mahamudu amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Julai 9,2022 na kusema kuwa marehemu amekutwa amekatwa eneo lake la shingoni,mkono pamoja na kifuani na kueleza kuwa chanzo kinasadikiwa ni wivu wa kimapenzi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi Kata ya Magata Karutanga Kijiji cha Kasheno eneo la Kaina wilayani Muleba mkoani Kagera wameelezea kusikitishwa kutokea kwa tukio la mauaji hayo yaliyopelekea kutokea kwa taharuki na kulaani vikali huku wakitoa wito kwa Jamii kutojichukulia sheria mkononi.Hata hivyo,taarifa zilizopo tayari mtuhumiwa huyo wa mauaji amekatwa akijaribu kutoroka.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma