skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mkoa wa Mwanza unatarajia kuanza kampeni ya  kuchanja wananchi wapatao 245,324 chanjo ya UVIKO 19 kuanzia June 16-22 mwaka huu ambapo jumla ya dose 324,000 aina ya Jensen zimesha sambazwa Katika halmashauri zote na vituo vya huduma ya afya.

Taaifa hii imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engineer Robert Gabriel wakati akizungumza na wadau wa afya, wakurugenzi, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Wilaya na Waandishi wa habari Katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (Picha kutoka Maktaba ya Buha FM)

Mhandisi Gabriel amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo ambao mapambano dhidi ya uviko 19 yakaendelea.

Wakurugenzi,Wakuu wa wilaya na viongozi wote hakikisheni mnafatilia na kuhamasisha wananchi sehemu zote ili waweze kupata chanjo kwani ni haki ya kila mtu“amesema mhandisi Gabriel.

Akizungumzia changamoto  amesema kuwa uingizaji takwimu kwenye mfumo ambapo hadi June 11 mwaka huu wananchi 813,1200 ambao wamechanjwa hawajaingizwa kwenye mfumo ambao unatoa taarifa kamili.

Niwapongeze Sana Wakuu wa wilaya na viongozi wote kusimamia na kusukuma mbele ufanikishaji wa Jambo hili kipekee niwapongeze Sana wilaya ya Ukerewe kwa kuchanja wananchi wengi waliopata  dose angalau mmoja ya uviko 19″ amesema RC Gabriel.

Kwa upande wake mratibu wa chanjo Mkoa Amos Kiteleja amesema kuwa kutokana na uviko kuleta madhara Katika jamii na mtu  ambaye hajachanja chanjo hiyo anaweza kupata kirahisi na wakati mwingine kupoteza maisha.

“Tangu tuanze kuchanja mwaka Jana June mpaka Sasa hivi tumeshachanja watu wengi Katika Mkoa wa Mwanza takribani watu 470,000 tumewafikia angalau dose ya kwanza na zaidi ya 300,000 tumeshawachanja dose ya pili”amesema Kiteleja.

Nae mganga  Mkuu Mkuu halmashauri ya Ukerewe  Dr Gitera Nyangi amesema kuwa zaidi ya 95% wamepata Katika halmashauri ya Ukerewe kwa kushirikisha jamii kwa kuwapa elimu na ushawishi kupitia viongozi wa ngazi ya kitongoji.

“Tunawapa motisha kazi ni ngumu ukiangalia Ukerewe visiwa ni vingi watu wanavuka maji kupanda mitumbwi kwa hiyo ni lazima utengeneze timu ya kufanya kazi zoezi lina tumia nguvu watu wapate motisha walau maji ya kunywa” amesema Dr Nyangi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Americares Tanzania Dr Nguke Mwakatundu amesema kuwa kupitia shirika hilo ambalo linaisaidia Serikali Katika utoaji wa madawa,kusaidia huduma za afya kwenye vituo vya afya pamoja na huduma za afya ya jamii.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma