skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz Β 

UCHAMBUZI WA NATIJA NA RAJUA

Anaaandika Ahmad Sovu PhD

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-kazi iendelee

Jumamosi na Jumapili hii zimeacha historia ya pekee kwa nchi ya Tanzania katika upande wa soka hususan mpira wa miguu.

Klabu kongwe na zenye mashabiki sifufu za Yanga na Simba zilivyoingia na kufanikiwa kufuzu kibabe katika hatua ya robo fainali katika mashindano yenye hadhi ya juu Afrika baada ya kutoka katika hatua ya makundi yale ya Klabu Bingwa Afrika na Shirikisho.

Simba na Yanga ni kama wamempa ‘hadiya’ zawadi Maalum Mheshimiwa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ametimiza miaka 2 madarakani.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa katika maadhimisho ya kupongezwa kwake na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) juzi tarehe 19/3/2023 Simba na Yanga wanahanikiza pongezi hizo kwa kushinda Kibabe katika michezo yao iliyowanya wafuzu.
Ambapo Simba waliichabanga timu ya Horoya ya Guinea kwa magoli 7 kwa nunge nao Yanga Afrika wakiitandika bila Huruma klabu ya US Monastir ya Tunisia kwa goli 2 kwa mojaπŸ˜˜πŸ‘πŸ‘ .

Milioni 5 za Rais Samia kwa kila Bao

Kabla ya mechi hizi kuchezwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan alitoa motisha ya kutoa zawadi ya Fedha Shilingi za Tanzania Milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa kwenye michezo hiyo

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametekeleza ahadi hii kwa vitendo na kwa hakika imechagiza sana mafanikio makubwa ya timu hizi na kuiingiza timu 2 za Tanzania katika hatua hizi kubwa za Kimataifa.πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ’š

Motisha za Mheshimiwa Rais Dkt.Samia
Kwa kutambua umuhimu wa motisha, hususan katika sekta ya michezo Dkt.Samia kwa mara kadhaa amekuwa akitoa motisha kwa timu zetu za Taifa na vilabu.

Mayele na wenzake wakishangilia ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Monastir ya Tunisia

Mathalan, katikaTimu ya Taifa ya wasichana wenye umri chini ya miaka 17, maarufu Serengeti Girls alitoa motisha ya kula nao na kuwapa zawadi kadhaa ambazo zilisaidia timu hiyo kufuzu na kupata fursa ya kushiriki kombe la dunia lililofanyika nchini India mwaka jana 2022 na kuweza kutinga hadi hatua ya robo fainali.

Ambapo Klabu ya Yanga na Simba tayari zimezawadiwa fedha zaidi ya Milioni 50 kwa kuzichabanga timu mbalimbali katika mashindano hayo.

Heko Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa motisha hii adhimu.

Natija za kufuzu hatua ya robo kwa vilabu hivi na nchi ya Tanzania

Kwa mujibu wa uchambuzi wa ndugu Yossima jr anasema:
Baada ya Simba kufuzu hatua hii tumefanikiwa kuongeza pointi 10 na kufikisha pointi 39 na kuwa na uhakika wa asilimia 100 wa kupeleka timu 4 tena msimu ujao
Kadhalika kufanikiwa kwa Yanga kuingia hatua hiyo kama nchi:

Tutakuwa tumeongeza pointi 7.5 na kufikisha pointi 46.5 na kupanda kutoka nafasi ya 9 ya association ranking mpaka nafasi ya 6 kama nchi tutakuwa lenye nguvu Afrika

Katika mafanikio haya tunazidi kujifunia Rais wetu Dkt.Samia kwani kupitia motisha zake pamoja na mipango ya klabu hizo zimetufikisha hapoπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ’š.

Hatua hii ya Dkt.Samia pia imesaidia zaidi Kuitangaza nchi Kimataifa katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Milioni 5 zilivyokuwa KIVUTIO

Msemaji wa serikali Ndugu Gerson Msigwa ambaye ndiye aliyekuwa akileta ‘mzigo’ 🀣🀣 yaani Fedha hizo za motisha imekuwa kivutio cha aina yake.

Fedha hizo zilikuwa zikitolewa fedha taslimu mara timu inaposhinda. Mwenyewe Msigwa alikuwa akisema Mama Hana mbambamba mzigo upo wa kutosha na kweli mizigo tumeiona.

Kivutio zaidi kilikuwa zaidi siku ya mechi ya Simba dhidi ya Horoya Ambapo Simba walimuadhibu Horoya goli saba kwa bila wenyewe wanaita wiki, seven upπŸ˜ƒπŸ˜ƒ Kuliibuka mizaha kadhaa kama vile: Simba wapunguze kasi. Hali ya hazina si nzuri🀣

Sasa Thimbwa leo mnataka mmalize hazina yote ya mama?? Sisi Yanga tutapewa nini kesho jamani?πŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Msigwa, mwambie refa amalize mpira, mi sina hizo helaπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Basi alimradi kulikuwa na mizaha ya aina mbalimbali yote kuhanikiza umuhimu wa motisha hii adhimu ya Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan kwa vilabu hivi.

Kama kwamba haitoshi, Mheshimiwa Rais akajibu mizaha hiyo na kuwaambia nyie endeleeni kuwafunga tu fedha zipo. Huyu ndio Dkt.Samia Suluhu Hassan Chifu Hangaya Mola amuweke.

Maoni/ushauri wetu wa jumla

Hapa ni dhahiri kuwa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonesha nia yake ya kuendeleza soka letu na kuitangaza nchi kwa ujumla wake. Hivyo tunaona inafaa kushauri mambo kadhaa kama vile;

-Viongozi wa Simba na Yanga waendelee kujiimarisha na kujizatiti vilivyo ili kuzidi kufuzu katika hatua ya nusu fainali na baadaye fainali.

  • Timu nyingine ikiwamo Azam, Namungo, Geita n.k kuendelea nao kujiimarisha ili kuzidi kuwa na timu nyingi zaidi katika michuano ya Kimataifa.

-Kuendelea na jitihada za Uboreshaji wa miundombinu ya Michezo nchi nzima ili kukuza zaidi soka na michezo mingine kwa ujumla.

Pia naipongeza Wizara ya UTASAMI kwa kazi kubwa waifanyayo ya kukuza michezo, sanaa na utamaduni wetu lakini pia wamekuwa mstari mbele na sako kwa bako katika kuhakikisha motisha ya Mheshimiwa Rais inawasilishwa ipasavyo.πŸ‘πŸ‘

Kongole sana Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuonesha njia na jitihada katika kukuza na kuendeleza michezo yetu na kuitangaza nchi yetu.

Mwandishi ni Mhadhiri na Mshititi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni DSM.

sovu82@gmail.com
0713400079

Back To Top
Buha FM Β· Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma