skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Felister Matinde Nestory – Muba FM Mwanza

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng Robert Gabriel amesimamisha utoaji wa mikopo ndani ya siku 30 katika Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza kwa lengo la kutoa elimu kanuni, Sheria na taratibu za mikopo.

AMheshimiwa Gabriel alisema hayo April 25 mwaka huu wakati akitoa ufafanuzi kuhusu fedha za mikopo ambazo serikali inatoa kwa vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu na kusema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya makundi hayo ambayo yatatakiwa kujikwamua kiuchumi.

RC Gabriel alisema kuwa mamlaka za serikali za mitaa zinatakiwa kuanza kutoa elimu kwa wananchi juu ya mikopo na urejeshaji ili kuijengea jamii yenye uaminifu katika kurudisha mikopo husika  kwa wakati

“kila halmashauri zimetengwa10% za pesa ya mapato ya ndani kwa ajili ya  vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na kila kikundi kitapaswa kuwa na watu kumi na kuendelea lengo likiwa ni kuwajengewa uwezo makundi hayo kiuchumi kwa mujibu wa Sheria” alisisitiza Mhandisi Gabriel Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Akizungumzia sifa za mikopo, mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema, wenye sifa za kupata mikopo ni Vijana, Wanawake na wenye ulemavu ambao wamejiunga katika vikundi na kikundi kiwe kimesajiliwa na kwamba idadi ya wanakikundi ni kuanzia watu kumi na kuendelea

“Kila kikundi kinatakiwa kirejeshe fedha za mikopo baada ya miezi mitatu tangu siku ya kupata mkopo na marejesho ya mkopo wanafanywa kila mwezi kwa kuzingatia viwango vilivyokubaliwa Kati ya mamlaka ya serikali za mitaa na kikundi kilichopatiwa mkopo “amesema Rc Gabriel.

“Endapo kikundi kitashindwa kurudisha fedha za mikopo katika muda uliopangwa mamlaka za serikali za mitaa itakipa kikundi hicho notes ya siku 30 ya kukitaka kikundi hicho kutoa sababu za kushindwa kurejesha mkopo huo kwa wakati”amesema Eng Gabriel.

Akizungumzia changamoto za mpango huo,  Mkuu huyo amesema kuwa ni pamoja na halmashauri mbili ambazo zimetoa fedha za mikopo kwa vikundi ambavyo havijasajiliwa ambapo takribani milioni 800 zimetolewa bila kuzingatia taratibu.

Halmashauri hizo ni pamoja na almashauri wilaya ya ukerewe iliyotoa shilingi milioni 55871850 na halmashauri ya wilaya ya Magu milioni 24132000 jumla milioni 800.

Ameongeza kuwa uamuzi wa serikali ya mkoa wa Mwanza kusitisha kwa muda utoaji wa mikopo ni pamoja na kubaini kwa uwepo wa wanavikundi wenye ajira rasmi waliopewa mikopo kinyume na Sheria ikiwemo wilaya za  Ukerewe,Magu,Misungwi Ilemela ambazo ni million 5944000 zilizotolewa kinyume na sheria, kutolewa kwa mikopo kwa vikundi ambavyo havina utambulisho kutoka kwa watendaji wa vijiji, mitaa pia vitambulisho  vya ujasiliamali.

RC Gabriel ameongeza kuwa bilioni 4933482619 ambazo ni sawa na 56% hazijarejeshwa kwa kipindi cha utoaji wa mikopo ndani ya  miaka mitatu.

Kwa upande wake karibu wa ccm mkoa wa Mwanza Peter Julius amesema kuwa fedha zote za mikopo hazina riba zirudishwe  kwa wakati katika mamlaka husika ili kuwasaidia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma