skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu, Kigoma

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Mwantum Mgonja Leo Julai 30, 2023 amefanya ziara Soko la Masanga kwa lengo la kukagua miundombinu na ufanisi wa Soko katika kuhudumia  Wakazi wa Manispaa hiyo

Katika ziara hiyo Mkurugenzi ameambatana na Mkuu wa divisheni ya Biashara na uwekezaji Bw. Robert Sabhoya na Mwekahazina wa Manispaa Bw. Osward Mwakalasi

Mkurugenzi wa Mansapaa Bi. Mwantumu Mgonja (kulia) akiteta jambo na maafisa wake Robert Sabhoya (kushoto) na Oswald Mwakalasi (katikati)

Katika ziara hiyo ya kutaathimini uwekezaji na kukagua mazingira ya biashara, Mkurugenzi huyo amekutana na Kuongea na  Mwenyekiti wa Soko Ndugu. Jafet John Nayingo  ambapo amemuelezea changamoto za soko hilo  na kuahidi kuzitatua

Mkurugenzi Mwantumu Mgonja akisikiliza maoni ya mwenyekiti wa soko hilo Bw. Japhet Nayingo

Bw. Nayingo amemweleza mkurugenzi kuwa mazingira ya soko ni mazuri japo kuna changamoto ndogo ndogo za uelewa ambazo zinatakiwa kutatuliwa kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu mifumo mbalimbali ya kiserikali

Aidha Mkurugenzi ameongea na mfanyabiashara mmoja mmoja huku akifanya ununuzi wa baadhi ya bidhaa ndani ya soko hilo na kufurahishwa na namna wakazi wa mansapaa ya kigoma wanavyojituma katika kufanya shughuli halali za kjkuza uchumi

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma