skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

FATAKI BACHINGE JAX, ni baba wa familia ya watoto wanne, ambaye aliingia nchini Tanzania akitokea nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zamani ikijulkana kama Zaire, Fataki ameingia Tanzania na kuanza kuishi katika makambi maalum akiwa na umri wa mika miinne tu.

Fataki ni kijana aliyeishi na ndoto ya utangazaji tangu akiwa mdogo, jambo ambalo pamoja na misukosuko ya ukimbizi bado aliendelea kuisimamia ndoto yake hiyo mpaka sasa, ambapo amefanikiwa kuingia katika tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.

Anasema jambo lingine lililochangia kwa kiasi kikubwa kujiendeleza na fani hiyo, ni aina ya maisha wanayoishi katika makambi, kwani wakati mwingine wanakosa mahitaji muhimu hali ambayo inamlazimisha mtu kutafuta njia za kujipatia kipato ili aweze kuyamuda masha.

Fataki anaongeza kuwa changamoto ni nyingi anazokutana nazo katika kazi ya uandishi wa habari hasa kutokana yeye kuwa mkimbizi lakini hakati tamaa katika kazi yake hiyo, kwani ndio inayomfanya sasa anapata chakula na familia yake.

Akielezea historia ya maisha yake anasema hatosahau, pale alipohadithiwa na wazazi wake kuwa katika harakati za kukimbia kutoka nchini Kongo, ndugu yake mmoja aliuwawa na makundi ya kigaidi, jambo ambalo anasema yeye na wazazi wake kufika katika makambi yaliyopo Kigoma ilikuwa kama ndoto.

Kwa sasa akiwa ni muandishi wa habari Fataki ameiomba serikali ya Tanzania kuendelea kuwasaidia wakimbizi waliopo katika makambi, ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza vijana ambao wanavipaji vya michezo mbalimbali pamoja na kuwapa uraia, baadhi ya wakimbi ambao wameishi kwa muda mrefu katika makambi ya Nyarugusu.

Sikiliza mahojiano na Fataki hapa chini kwa kubonyeza kitufe hapa chini

Simulizi ya FATAKI kuoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma