skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Bariadi

Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linamshikilia Bi. Salu Magambo mkazi wa mtaa wa Mwaswale wilayani Bariadi mkoanii Simiyu kwa tuhuma za kumuua mme wake.

Akitoa taarifa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari mkoani Simiyu kamanda wa jeshi hilo mkoani hapo ACP Blasius Chatanda amesema tukio hilo limetokea April 2, 2023 majira ya saa 4:30 asubuhi mtaa wa Mwaswale kata ya Sima wilayani Bariadi ambapo mtuhumiwa anatajwa kumuua mume wake aliyefahamika kwa jina la Boniphace Upepo.

Kamanda Chatanda amesema Boniphace Upepo aliuawa kwa kunyongwa na waya shingoni na kisha mwili wake kutupwa kwenye korongo lenye maji mita chache kutoka nyumabani kwao.

Marehemu Boniphace Upepo alikuwa anaishi na mpenzi wake Salu Magambo,siku ya April 1,2023 walikuwa wote katika mgahawa wa mpenzi wake uliopo mtaa wa Sima, waliondoka kwa pamoja kwenda nyumbani kwao mtaa wa Mwaswale na hawakuwa na ugomvi wowote ” amesema kamanda Chatanda.

Kamanda Chatanda amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa awali umebaini marehemu alikuwa akiishi na mkewe, na walikuwa na ugomvi na mpenzi wake ambapo walikuwa wanadaina pesa hali hiyo ilipelekea ugomvi na kufikishana kwa mwenyekiti wa mtaa wa Mwaswale kuomba msaada wa kisheria jinsi ya kulipana pesa hizo.

Kwa mujibu wa kamanda Chatanda mahojiano ya awali mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo kwa kushirikiana na wenzake ambao bado jitihada za kuwatafuta zinaendelea ili kujibu tuhuma zinazowajabili .

Kamanda Chatanda amesema Uchunguzi pia ulibaini mwili ulikuwa na michubuko shingoni na ulionekana uliburuzwa mpaka kwenye hilo korongo na mahojiano kuhusiana na tukio hilo bado yanaendelea, na mara baada ya kukamilisha taratibu za kiupelelezi jalada litafika ofisi ya taifa ya mashitaka mkoa kwa hatua za kisheria

Awali viongozi wa mtaa na wananchi akiwemo mwenyekiti wa mtaa wa Mwaswale Emmanuel Mabula wamesema mke wa marehemu baada ya tukio kutokea alifunga biashara na kutoweka na kabla ya kifo hicho walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara.

Jeshi la polisi mkoani hapo limewataka wananchi mkoani hapo kutojichukukia sheria mkononi kwani kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Bariadi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu tukio hilo kama wanavyoeleza katika viteo hapa chini

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma