Waandishi wa habari wa Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma wametakiwa kutumia Takwimu za sensa…
Adela Madyane-Kigoma
Imeelezwa kuwa kati ya wajawazito 10 wanaohudhuria kliniki wilayani Kasulu mkoani Kigoma wawili kati yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18
Hayo yameelezwa na Robert Rwebangira mganga mkuu wa wilaya ya Kasulu wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa vya hedhi salama kwa wanafunzi wa sekondari ya Makere iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma
“Inasikitisha sana kuona watoto wadogo wanajiingiza katika mapenzi ya utotoni kwakuwa yapo madhara makubwa yanayoambatana na vitendo hivyo si tu wakati wa kujifungua bali hata kwenye hatua nyingine za ukuaji” Amesema Rwebangira

Akitaja baadhi ya madhara yanayotokana na kufanya mapenzi utotoni amesema ni homa ya ini pamoja na kansa ya shingo ya uzazi na kuitaka serikali idara ya elimu kuongeza club za mimba za utotoni mashuleni ili wapate elimu ya afya ya uzazi wangali watoto wadogo
Naye Yahaya kwatte Mratibu wa wa afya ya uzazi na mtoto ameitaja Shunguliba kuwa kata niayoogoza kwa mimba za utotoni yenye asilimia 56 ya watoto wanaoshika ujauzito chini ya umri na kuwaomba wazazi kusimamia malezi ya watoto ili kunusuru kizazi kijacho
Akizungumzia sababu ya mimba za utotoni diwani wa kata ya Makere Laurent Kilali ametaja kuwa ni filamu za ngono zinazooneshwa kwenye kumbi za video pamoja na kwenye simu za wazazi ndio vyanzo vikuu vya changamoto hiyo
Amesema zaidi ya watoto 300 waliohojiwa katika tafiti za ndani kuhusiana na filamu za ngono wote wameshaona kupitia maeneo hayo mawili na kuzitaka mamlaka kuacha kuonesha filamu hizo kwenye uwepo wa watoto na wazazi kuacha kutunza filamu hizo kwenye simu
“Watoto wakiona filamu hizo wanashikwa na hamu ya kujaribu kile walichokiona, tusiwaweke watoto kwenye tabia zitakazo hatarisha maisha yao ni hatari kwa kizazi kijacho” amesema diwani huyo
Aidha Monica Francis afisa ustawi wa wilaya amewataka wanafunzi kujifunza zaidi juu ya afya ya uzazi na kujikinga na kila kiashiria cha mimba na kwamba wasikibali kwenda kwenye masoko ya usiku kwani ni chanzo cha kukutana na wavulana na kuingia katika vishawishi