Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais…
Kamati ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya Bunge la Ujerumani leo imefanya ziara maalumu nchini Tanzania na kuzindua mradi wa pamoja wa kudhibiti taka na kuhifadhi mazingira mkoani Kigoma.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 28 umefadhiliwa na serikali ya ujerumani kupitia kwa balozi wa Ujerumani nchini Tanzania ambao wametoa kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 23 kwa ajili ya kujengea uwezo vikundi vya vijana kuzalisha bidhaa mbadala kutoka katika vifaa mbalimbali vilivyoisha matumizi yake hususani magurudumu ya magari pamoja na mifuko ya sandarusi inayohifadhi saruji na chokaa.

Akitoa Maelezo kuhusu mradi huo, Kiongozi wa msafara wa wabunge hao Bw. Knut Gerschau kutoka chama cha FDP amesema Ujerumani inafarijika kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi yenye faida za moja kwa moja kwa wananchi na kwamba ujerumani inatarajia kuwa licha ya mradi kuendeleza usafii wa mazingira pia vijana wengi watapata ajira.
Mratibu wa kituo hicho kinachoratibiwa na kampuni Africraft Tanzania Bw. Kelvin Nicholaus amebainisha kuwaufadhili wa ujerumani umewezesha kujengwa kwa karakana na kituo cha vijana na takribani vijana 60 watapatiwa mafunzo na uzalishaji mali kutokana na taka mbalimbali.
Milka Ashel ambaye ni mmoja kati ya vijana ambao tayari wamepata mafunzoo ya utengenezaji wa mikoba ya aina mbalimbali inayotokana na vifuko ya sandarusi kwa kunakshiwa na vitenge, amekiri kuwa Ufadhili wa Ujerumani umekuwa mkombozi kwake kiuchumi.

“Kwangu mimi hii ni ajira mhimu, hapa najipatia kipato na kujikimu kimaisha, unajua wapo wasichana kama mimi ambao hata kupata miambili au mia kwa siku hawawezi, hivyo kituo hiki ni mhimu sana kwetu, Nawashukuru wabunge wa Ujerumani na Balozi Regine Hess kwa kutujali” alisisitiza Milka Ashel mnufaika
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo ameishukuru Ujerumani kwa ushirikiano wake katika kufadhili miradi mbalimbali nchini Tanzania.

“Ujerumani imekuwa ni mdau mhimu kwa Tanzania hasa katika kufadhili miradi ya maendeleo kwenye sekta za maji na mazingira” amesisitiza Andengenye
Kwa upande wake askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste motomotoTanzaniaAskofu Ezra Enock ambaye ndiye aliyeshawishi mradi huo kuanzishwa Kigoma na kisha kufadhiliwa na Ujerumani amesema Kigoma kuna vijana wengi wenye vipaji lakini hawakuwa na taasisi ya kuwajengea uwezo

Jumla ya wabunge sita wanaounda Kamati ya bunge ya ushirikiano wa kiuchumina maendeleo kutoka vyama vya SPD, AfD, CDU/CSU, FDP, na Die Linke vya Ujeruman wako ziarani nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine wataitembelea Meli kongwe ya MV Liemba iliyotengenezwa Ujerumani Zaidi ya miaka 100 iliyopita.