Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na. Matinde Nestory
Wadau wa sekta ya madini wamekutana jijini Mwanza kwenye jukwaa la kwanza la utekelezaji na ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Madini.
Jukwaa hilo limefanyika Rocky City Mall jijini Mwanza likiongozwa na mwenyekiti wa tume ya madini profesa Idrisa kikula ambaye amemwakilisha waziri wa Madini mheshimiwa Doto Biteko
Professa Kikula amesema kuwa sekta ya Madini imefanya mabadiliko ya Sheria ambayo yamepekekea kutungwa kwa kanuni za ushirikishwaji wa Tanzania za mwaka 2018, na kwamba lengo kuu ni kuibua na kuchochea kuongezeka kwa fursa mbalimbali za ajira na matumizi ya huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.
” Katika kipindi Cha kuanzia mwaka 2018 -2021 sekta ya Madini imeongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha ushirikishwaji watanzania katika maeneo mbalimbali ajira na mafunzo kwa watanzania katika migodi mikubwa na Kati ambapo kumekuwepo na ongezeko la ajira 6668 sawa na 95% kwa mwaka 2018 hadi kufikia 14308 sawa na 97% za mwaka 2021

Anasisitiza kuwa ongezeko hilo la ajira kwa watanzania limechochewa na usimamizi wa ushirikishwaji watanzania wamepewa kipaumbele katika fursa za ajira zote nchini.
Akizungumzia changamoto amesema kuwa baadhi ya makampuni ya kigeni hayajaweza kukidhi matakwa kwa kuingia ubia na wachimbaji wa Tanzania na kwamba hali hiyo imepelekea kampuni za wazawa kokosa sifa, upungufu wa viwanda nchini kwa ajili ya uchimbaji na uchenjuaji nchini, wamiliki wa leseni na watoa huduma kutokutekeleza matakwa ya uchenjuaji kwa kushindwa kufanikisha mpango wa ushirikishwaji, kushindwa kufata taratibu za manunuzi.
Nae Bi. Janeth Reuben ambaye ni kamishna wa ushirikishwaji tume ya madini amesema kuwa tume ya hiyo iko kwa ajili ya kujadili na kujengeana uwezo wa kujua rasilimali dhahabu na Madini mengine na jukwaa hili litakuwa linafanyika kila mwaka ili kujua changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.