skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory- Mwanza

Wananchi mkoani mwanza wametakiwa kutekeleza kwa vitendo dhana ya uzalendo,uadilifu na kufanya kazi kwa bidii katika kulinda rasilimali za taifa, kupambana na kuzuia rushwa, kupambana na ujangili wa wanyama pori pamoja na kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa iliyofanyika katika mnara wa mashujaa kutoka kanda ya Ziwa uliopo eneo la mzunguko jijini Mwanza.

Mhandisi Gabriel amesema kuwa jamii inatakiwa kulinda rasilimali za taifa la Tanzania katika kuleta maendeleo kwa kuimalisha Miundo mbinu ya barabara, maji,nishati,elimu,afya pamoja na mshikamano hali ambayo itasaidia kutowanufaisha watu wachache.

Mzee Bega Maliba mwenye umri wa miaka 104  Askari yaliyepigana Vita ya pili ya dunia.

“Mashujaa hawa walipanda mbegu ya utaifa,uzalendo,ukakamavu,upendo, amani na mshikamano kwa jamii zao walipoteza maisha yao kwa ajili ya kutetea,kupigania na kuulinda Uhuru wa Tanzania na mbinu walizotumia mababu Zetu hawa zimeendelea kuboreshwa na kuendelezwa kwa mbinu za kisasa za kulinda Uhuru wa mipaka na rasilimali za taifa letu”amesema Mhandisi Gabriel.

Ameongeza kuwa kumbukumbu za mashujaa zimewezesha kizazi Cha Sasa na kijacho kujifunza namna ya kuendeleza amani na umoja na kulinda rasilimali za taifa la Tanzania.

Hata hivyo amesema kuwa Tanzania uadhimisha siku ya kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha yao katika Vita ya kwanza ya dunia 1914-1918 na Vita ya pili ya dunia1939-1945 wakitetea, kulinda na kupigania Uhuru wa Tanzania kila ifikapo July 25 ya kila mwaka.

Picha Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akiwa na viongozi mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Amina Makilagina katibu tawala Mkoa wa Mwanza Ngussa Samike (mwenye tai) na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo.

Mhandisi Gabriel aliyeambatana na viongozi wengine wa Mkoa wa Mwanza na mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Athony Dialo amewakumbusha wananachi kujitokeza katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Aug 23 Mwaka huu

Nae mmoja wa Askari aliyepigana Vita ya pili ya dunia Mzee Bega Maliba mwenye umri wa miaka 104 anayeishi wilaya ya Ukerewe amesema kuwa alitokea Musoma Tanzania na kufika Nairobi nchini  Kenya ambapo ambapo aliungana na wapiganaji wengine kutoka mataifa mbalimbali kwenda kushiriki vita hivyo vilivyotajwa kuwa ni dhidi ya Adolf Hitra.

Mzee Bega amesema kuwa pamoja na kazi kubwa na ngumu waliyoifanya kwa sasa wanaishi maisha magumu kutokana na kutopata pesa za kujikimu kutoka kwa serikali na kwamba hapo awali wamekuwa wakipata malipo kidogo kutoka kwa malkia Elizabeth wa Uingereza lakini muda umepita bila kulipwa chochote.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma