skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wakati vijana wengi wakikimbilia kuchenza kamali kwa utumiaji wa fedha aina ya sarafu kwa kucheza bahati nasibu katika kile kinaotajwa kuwa ni bonanza ambapo wengi huishia kutoka machoni baada ya kupoteza maelfu ya pesa zao, Jumla ya mashine 24 za michezo ya kubahatisha zenye thamani ya zaidi ya Tshs. milioni 36 ziliharibiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha mkoani Kigoma baada ya msako mkali uliofanywa na bodi hiyo kwa kushirikiana na askari polisi Januari 2022.

Bodi imefikia hatua ya kuharibu mashine hizo kutokana na kukiuka sheria ya michezo ya kubahatisha ya mwaka 2003 kifungu cha 4 na wamiliki kushindwa kufika ndani ya siku 7 kueleza sababu za kuziweka mashine hizo katika maeneo waliyokutwa.

Akizungumzia suala hilo mkurugenzi mkuu wa bodi ya taifa ya michezo ya kubahatisha James Mbalwe amesema mashine zilizokamatwa zimekutwa katika maeneo yasiyostahili na ni kinyume cha sheria kufanya biashara hiyo bila kusajiliwa.

“Waendeshaji wa michezo ya kubahatisha waweke mashine zao kwenye tovuti zilizosajiliwa na bodi, wamiliki wawe na vibali vya uendeshaji na mashine zisajiliwe kwa kushindwa kufanya hivyo, jambo ambalo linaonekana kuwa ni ukiukwaji wa sheria za nchi,” alisema Mbalwe. p>

Akifafanua zaidi alisema, kwa mashine 24 zilizoharibika serikali imepoteza zaidi ya milioni 2.6 kwa mwezi ambapo mashine moja inatakiwa kulipwa t.sh 110,000 kwa mwezi gharama inayojumuisha kodi na ada ya miamala na ile kwa mwaka. sekta ya nafasi inachangia takriban bilioni 25 kwenye Pato la Taifa

Mkurugenzi huyo alitaja maeneo ambayo mchezo huo hauruhusiwi kuchezwa ni pamoja na shule, nyumba za maombi, majengo ya hospitali, makazi ya watu, pamoja na maeneo ya usalama wa taifa hadi sasa bodi hiyo imefanikiwa kusajili mashine 17,000 kwa kufuata sheria na sera za nchi.

Akizungumza kwa niaba ya jamii Yusuph Musa amefurahishwa na kitendo cha serikali kuharibu mashine hizo kwani zinaharibu maendeleo ya kisaikolojia ya watoto na kuzorotesha elimu yao

Watu wengi wanaocheza kwenye mashine hizi ni watoto chini ya umri wa miaka 18, wanatuibia fedha wakikuta zimebaki 200 wanazichukua kwa ajili ya mchezo, wanapotea kielimu na maadili yanazidi kudorora” Alisema Musa.

Kwa upande wake Anton John ameitaka serikali kuendelea na zoezi la kuharibu mashine hizo na kuhakikisha taratibu zote za mchezo huo zinafuatwa ipasavyo.

Imeandikwa na Adela Madyane- Kigoma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma