skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke ameiomba serikali kuangalia upya vyeti vya ndoa vya Baraza Kuu la waislamu (Bakwata) vitambulike kisheria pindi wanapohitaji msaada viweze kuwasaidia.

Hayo yamebainishwa jana katika swala ya Eid Al  Hajj iliyofanyika katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza ambapo mamia ya waislaam waliungana na wenzao duniani kusherehekea sikukuu hiyo mhimu inayoenda sambamba na Hija.

Sheikhe Kabeke amesema kuwa serikali itambue vyeti hivyo ambavyo vimekuwa vikipelekwa kwa ajili ya kuomba uhamisho au kupandishwa vyeo vinakataliwa na kuombwa Cheti Cha serikali.

“Haiwezekani ndoa ya Kiislam inatambulika kwa mujibu wa Sheria halafu Cheti kinachothibitisha hii ndoa imefungwa hakikubaliki serikalini”amesema Sheikhe Kabeke.

Sambamba na hayo amesema kuwa  waislam wahakikishe wanafunga ndoa kwa taratibu na misingi ya dini ya kiislam hii itasaidia Kupunguza matukio ya kikatili ndani ya ndoa yanayosababishwa na mfumo holela wa ndoa.

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika viwanja vya Nyamagana kusherehekea sikukuu ya Eid maarufu kama sikukuu ya kuchinja iliyofanyika July 10

Hata hivyo ameiomba serikali iondoe zuio hilo ambalo limesababisha jamii ya kiislam kukosa haki za kuhamishwa au kupandishwa cheo.

Sanjari na hayo Sheikhe Kabeke amewakumbusha wananchi kujitokeza kwenye zoezi Zima la sensa la watu na makazi ambalo linatarajia kufanyika Aug 23 mwaka huu.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi  amewataka wazazi na walezi kuwalinda watoto katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid pamoja kuwataka madereva na watumiaji wote wa barabara kufuata Sheria za barabarani na kuzingatia matumizi sahihi ya barabara.

Ameongeza kuwa mkoa wa Mwanza hali ya Ulinzi na usalama uko salama pamoja na kuwakumbusha wazazi kutembea na watoto wao katika kipind hiki cha sikukuu hali ambayo itasaidia kupunguza ajali zisizo na lazima.

Nae Mkuu wa wilaya ya Nyamaga Amina Makilagi amewataka wananchi wa wilaya ya Nyamagana kujiandaa Kuhesabiwa  Aug 23 mwaka huu pasipo  kuwa  na kikwazo kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Hata hivyo amewataka wananchi mkoa wa Mwanza waendelee kudumisha amani,umoja na usalama wa taifa la Tanzania.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma