Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Waandishi wa habari,wakurugenzi wa vyombo vya habari na wadau wa mawasiliano kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa wamekutana jijini Mwanza kwenye kikao kazi Cha kujadili utendaji kazi na changamoto za sekta ya mawasiliano.
Kikao kazi hicho cha majadiliano kimefanyika leo katika jijini Mwanza kikiendeshwa na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt Jabiri Bakari
Dkt Bakari katika kikaoo hicho cha kanda ya ziwa amesema kuwa wadau wa habari na watoa huduma za mawasiliano wamekuwa wakikutana kujadili utendaji kazi na kujua changamoto katika sekta ya mawasiliano na kupata ufumbuzi.
Katika maelezo yake ya kina amebainisha kuwa watoa huduma wa Mawasiliano na habari kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa wamewasilisha changamoto wanazokabiliana nazo kama watoa huduma wa mawasiliano katika jamii.

Mmoja wa wadau wa sekta ya mawasiliano Bw. Edwin Soko ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habarii mkoa wa Mwazna (MPC) amesema kuwa tozo na gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa jambo linalosababisha vyombo vya habari kushindwa kuajiri wanahabari wenye sifa stahiki.
Bw. Soko ametumia fursa hiyo pamoja na mambo megine kuiomba mamlaka hiyo kuangalia upya suala la kupunguza tozo ambayo itasaidia vijana wengi kujiajiri kwenye runinga za mtandao (online Tv) na kuajiri vijana wengine.
Ameongeza kuwa leseni imekuwa ikilipwa kwa dola, mitambo ya kurushia matangazo hutozwa ushuru na kodi nyingi, pamoja na tozo nyingine nyine na ameiomba TCRA kuanza mchakato wa kuzifuta kanuni ambazo zinahalalisha kuwepo kwa ushuru vifaa vya mawasiliano ya habari hasa vya runinga na radio
Aidha ameomba mamlaka hiyo kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari na wamiliki wa kurasa za habari mtandaoni ikiwemo runininga za mitandaoni ili kuongeza ufanisi na boresha biashara za habari nchini.
Akijibu hoja mbalimbali Mkurugenzi Dkt Bakari amesema kwa TCRA kushirikiana na wadau wa mawasiliano wataendelea kuimarisha ushirikiano sambamba na kutatua changamoto zinazobainika.