skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC

Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais wa awamu ya 5 hayati Dr. John Joseph Pombe Magufuli, MjMje wawa mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Hayati John Pombe Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kimataifa toleo la tatu, inayotolewa na taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu maarufu M. T. Kasalu, kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania na kwa Hayati Rais Magufuli akiwa Rais wa Awamu ya Tano wakati akitekeleza majukumu yake Kitaifa na Kimataifa.

Aidha, Tuzo hii hutolewa kwa Wenza “spouses’ wa Viongozi Wakuu wa Nchi na watu Maarufu duniani kwa kutambua michango yao kwa Wenza wao, jamii na Taifa husika.

Tuzo hii ifahamikayo zaidi kama M. T. Kasalu, Femme D’Honneur Trophee, ilitolewa jana Ijumaa tarehe 24 Machi, 2023 katika hoteli ya Pullman jijini Kinshasa.

Mama Janet Magufuli aliyesimama katikati akipokea tuzo Jijini Kinshasa nchini DRC

Waandaaji wa Tuzo hii ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakishirikiana na Taasisi ya Lizadeel.

Kwa mwaka huu waliopokea tuzo hii ya M. T. Kasalu, toleo la 3 ni;

  1. Mama Janeth MAGUFULI – Tanzania – mchango wake kwa Rais wa Awamu ya Tano unafahamika Afrika na duniani kote.
  2. Mama Suzanne MUKAY – Congo Mke wa Daktari maarufu nchini DRC, wa magonjwa ya kina Mama na kansa, mumewe ameisaidia jamii kwenye nyanja hizo.
  3. Mama Vivianne DALO – Mke wa Mchungaji Maarufu na anayeheshimika nchini DRC, Pastor Roland Dalo. Amesaidia jamii hasa wajane, yatima na vijana katika kujitegemea.
  4. Mama Colette SENGHOR mke wa Rais wa kwanza wa Senegal, Mhe. Leopold Sedar Senghor , aliisaidia Senegal kupata Uhuru.
  5. Mama Coretta KING mke wa Martin Luther King, USA. Mumewe alisaidia mengi ikiwemo kupinga ubaguzi wa rangi USA.

Akihutubia waumini katika misa maalumu ya kumbukumbu ya miaka miwili tangu kufariki kwa Dr. Magufuli, iliyofanyika leo jijini Mwanza Tanzania, spika mstaafu wa Bunge la Tanzania Mama Anne Makinda amemtaja Hayati Magufuli kama shujaa wa mageuzi katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu.

“Mara kwa mara nikimuwaza Magufuli namuona kama Rais aliyeletwa na Mungu, nimekuwa mtumishi wa serikali kwa miaka 40, nilishiriki shughuli nyingi za maendeleo na kushuhudia miradi mingi iliyobuniwa na kushindikana lakini Magufuli alifanya, mfano mradi wa umeme wa bwawa la mwalimu Nyerere tangu 1975 ulifikiriwa lakini hakuna aliyeujenga ila yeye alianza, miradi ya barabara, madarasa, vituo vya afya nk

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma