skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory – Mwanza

Umoja na ushirikiano ndio nguzo ya maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii, kisiasa pamoja na ulinzi na usalama ambao ndio chachu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima wakati wa makabidhiano ya madaraka na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mapema jana.

RC Malima amesema kuwa ushirikiano,ubunifu na umoja ndio Chachu ya maendeleo ya Mkoa wa Mwanza ambao ni Mkoa wa kimkakati wa biashara katika kuinua uchumi wa jiji la Mwanza na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amewaomba viongozi kuhakikisha mapato yanapatikana Mkoani hapa kwa kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri za jiji la Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima akikabidhiwa madaraka na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.

“Kama hivi tulivyokabidhiana sio Mara ya kwanza Mimi na yeye tunakabidhiana niliwahi kumkabidhi Mkoa wa Mara nilimkabidhi jumanne,jumatano ikapita tukaamka Alhamisi asubuhi kateuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Gabriel ni rafiki yangu Sana alikuwa Kiongozi wetu wakiimani na kiroho”amesema RC Malima.

Nae Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya amesema kuwa anawaomba viongozi na wananchi kwa ujumla kushirikiana ili kufanikisha gurudumu la maendeleo katika Mkoa wa Mwanza na taifa linafanikiwa pamoja na Mkoa wa Mwanza unakua kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa anashukuru viongozi na wananchi kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote Cha uongozi wake.

Ameongeza kuwa anawashukuru Viongozi wa kamati ya amani Mkoa wa Mwanza walioshirikiana katika kipindi Cha uongozi wake na kuwataka viongozi kuongeza juhudi katika kazi kwa kutumikia wananchi na taifa la Tanzania.

“Viongozi wa dini wamekua mstari wa mbele kuombea taifa la Tanzania na kumuombea Rais Samia nawasihi zidisheni maombi kuliombea taifa letu lizidishe amani na utulivu na kumuombea Rais wetu ndio maana nimeona heshima ya nchi yetu inajulikana mataifa mbalimbali taifa letu linazidi kupiga hatua”amesema Mkuu wa Mkoa mstaafu  mhandisi Gabriel.

Amesisitiza kuwa viongozi pendeni taifa la Tanzania,ukipewa dhamana ya kuongoza toa maisha yako kwa nchi ili kuipa heshima Taifa,tenda haki,pambana na udhalimu,simamia haki,tetea wanyonge,usiendekeze rushwa unasaliti taifa,kuwa msaada kwa taifa,litakie mema taifa la Tanzania pamoja na jivunie kuwa mtanzania.

Sanjari na hayo sherehe hizo za makabidhiano ya madaraka imeudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, kamati ya amani,wabunge,viongozi wa chama Cha mapinduzi (CCM),Wakuu wa wilaya, mnec,meya, Wazee,Wastaafu wa ukuu wa Mkoa,taasisi mbalimbali na wakurugenzi wa halmashauri.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma