skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Juungano wa Tanzania mheshimiwa Dk. Philip Isdor Mpango ameiagiza wizara ya mambo ya ndani kuacha kuwabughudhi wananchi wa Kigoma kuhusu uraia kutokana na wao kuwa mkoa wa mpakani na badala yake washughulikie masuala hayo kwa ustaarabu na kuzingatia maadili huku akisisitiza kuwa kuzaliwa Kigoma hakumaanishi kuwa sio raia.

Makamu wa rais mheshimiwa Dk. Philip mpango ametoa maelekezo hayo wakati akihutubia wananchi mjini Kigoma na kuwaagiza wabunge wa mkoa wa kigoma kukutana na idara ya uhamiaji ili kupanga namna bora ya kuwahudumia wananchi.

Aidha Makamu wa rais ambaye pia alizindua jengo la ofisi ya takwimu amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa corona kwa Kigoma ni miongoni mwa mikoa kumi inayoongoza kuwa na wagonjwa wengi.

Kwa upande wake waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mh. Profesa Joyce Ndalichako akisoma hotuba kwa niaba ya waziri wa fedha amesema wizara inaendelea na maandalizi ya sensa ya majaribio mwezi august ikiwa ni maandalizi ya sensa kuu ya watu na makazi 2022.

Sikiliza sauti hapo chini

Sauti ya Buha- Makamu wa Rais, Dr. Mpango ziarani Kigoma

Mwandishi: Kadislausi Simon- Kigoma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma