Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na Anita Balingilaki,Bariadi
Mwanamke mmoja amepoteza maisha baada ya kudumbukia kwenye dimbwi lililokuwa limejaa maji yanayotokana na mvua inayoendelea kunyesha wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Tukio limethibitishwa na kaimu kamanda mkoa, jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu Inspekta Faustin Mtitu akiwa eneo la tukio huku akimtaja jina mtu huyo kuwa ni Geuza Masunga, (57) mkazi wa mtaa wa Nyangaka kata ya Bariadi tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi mkoani Simiyu, ambapo mwili wa mwanamke huyu ulikutwa ukielea alfajiri ya Mei 2,2023 kwenye dimbwi hilo lililojaa maji ambalo lilichimbwa kwaajili ya kupata molamu ya kujengea barabara.

“Dimbwi hili lifukiwe,ili tusiendelee kupata vifo,tukitoka hapa tutaenda kukaa na viongozi wa wilaya lakini pia watu wa mtaa huu na mamlaka nyingine zinazohusika utengenezaji wa dimbwi hili tuone namna gani tunaweza tukaliondoa lisiwepo”amesema Inspekta Mtitu .
Aidha Inspekta Mtitu amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhali hususan kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha .
Rashid Zongo ni afisa tarafa ya Ntuzu amesema kama serikali watahakikisha jambo hilo halitokei tena, huku akiongeza kuwa jeshi la polisi linaenda kufanya uchunguzi ili kubaini kama kifo chake kinatokana na kutumbukia kwenye dimbwi.
wakazi na viongozi wa mtaa wa Nyangaka wamekuwa na maoni tofauti kuhusu tukio wengine wakiomba serikali kuliwekea uzio na wengine wakitaka lifukiwe.
“Hapa unakuta wengine wanakuja kufua lakini kwa huyu siwezi kujua ilikuwaje akadumbukia,mi ndio nilitoa taarifa kwa mweyekiti nimepita nikaukuta mwili” Peter John mkazi wa Nyangaka.
Kwa mujibu wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha Jan mpaka Mei 2,2023 ni matukio ya vifo vitokanavyo na maji ni 11.