skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi Dr Angelina Mabula amezitaka Taasisi za kidini ,watu binafsi ,Taasisi za umma ambao ni wadaiwa sugu kuanzia miaka Tano na kuendelea  kulipa madeni ndani ya July-Dec mwaka huu hali ambayo itasaidia kutolipa riba ya 1% ya tozo ya Kodi ya pango la ardhi.

Rai hiyo imetolewa leo katika mkutano wa ufafanuzi wa utekelezaji wa vipaumbele katika wizara wa mwaka 2022-2023 na  Waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya jiji la mwanza.

Waziri Mabula amesema kuwa wadaiwa wametakiwa kulipa madeni  hayo ndani ya miezi hiyo zaidi ya hapo watalipa na riba ya 1% ambapo wasipofanya hivyo watapelekwa kwenye vyombo vya Sheria.

Akitoa ufafanuzi wa vipaumbele katika utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022-2023 ni kuimarisha matumizi ya Tehama katika ofisi za Ardhi za Mkoa na halmashauri zote nchini,usalama wa miliki za ardhi,kuimarisha miundombinu ya upimaji wa Ramani,kujenga ofisi za ardhi za mikoa,kutoa hatimiliki 150,000 katika halmashauri 10.

Ameongeza kuwa urasimishaji makazi,mabaraza ya ardhi na Nyumba ambapo wameandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 50 katika wilaya 6 na Mipango ya matumizi ya ardhi ya wilaya pamoja na migogoro ya ardhi,utawala bora, tume ya Taifa  pamoja na shirika la Nyumba la Taifa 

Sanjari na hayo amebainisha kuwa migogoro katika wizara ya ardhi, wizara inatatua na kudhibiti migogoro kwa kutumia njia ya kuwashirikisha wadau wa ardhi katika kubadili nyaraka za upangaji,upimaji na umilikishaji ardhi kutoka analogia kuwa digitali Kama mpango wa muda mrefu katika kupunguza migogoro kwa kuwapa elimu umma kwa kushirikiana na wadau wa ardhi katika kupanga ,kupima na kumilikisha ardhi.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Rais Samia  Suluhu Hassan ambaye alisema hataki kusikia migogoro ya ardhi inayoendelea kwa hiyo tunapohamisha kutoka analogia kuingia digitali tunakwenda kukidhi mahitaji ya watanzania”amesema Waziri Mabula. 

Vilevile amesema kuwa mabaraza ya ardhi ya Kila wilaya ,Mkoa au Kanda yamerahisisha upatikanaji wa makala  kwa njia ya mtandao katika utawala bora,uwajibikaji,uwazi na ufanisi katika kutoa ufanisi wa kisekta kwa kuwezesha  uratibu mipango mbalimbali ya ardhi pamoja na halmashauri kukamilisha  takwa la kisheria la mwaka 2022-2023.

“Tumewezesha mabaraza mapya 59 kwa kutoa huduma katika wilaya zote nchini,kuimarisha ujenzi wa mfumo wa kusimamia Mashauri katika maabara ya ardhi kwa kutunza kumbukumbu za mashauri”amesema Waziri wa Ardhi Mabula.

Hata hivyo amewataka wananchi anaoishi  katika maeneo ambayo hayajapangwa kuendelea kushiriki  kikamilifu katika zoezi la urasimishaji ardhi ambalo ukomo wake  ni mwaka 2023.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma