Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na Anita Balingilaki, Bariadi
Serikali wilayani Bariadi mkoani Simiyu imeanza utekelezaji wa agizo la waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa alilolitoa Machi 26, 2023 la kuruhusu magari madogo (michomoko) kufanya kazi za usafirishaji wa abiria.
Waziri mkuu Majaliwa aliruhusu magari hayo kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kubeba abiria kwa kuzingatia idadi ya viti sambamba na kwenda mwendo unaotakiwa kisheria.
Simon Simalenga ni mkuu wa wilaya ya Bariadi amesema wilaya hiyo imeanza taratibu za utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu alilolitoa wakati akiongea na mamia ya wakazi wa mji wa Bariadi wakiwemo waendesha magari hayo akiwa safarini kuelekea wilayani Maswa kwenye ziara yake ya kikazi.

Simalenga amesema madereva wote wa magari madogo(michomoko) watatakiwa kutambulika na mamlaka husika LATRA kwa kupewa leseni ya usafirishaji, yakatiwe bima na yatawekewa alama maalum (mstari) ambao utaonesha gari hili linafanya safari kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine (inatoka wilaya ya Bariadi).
Tazama channel ya Buha Online TV hapa chini au tembelea ukurasa wetu wa You Tube kwa kubonyeza hapa
Kwa upande wake afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) mkoa wa Simiyu,Nicolas Kamzora amewataka madereva kusajiliwa ili kukidhi vigezo vilivyowekwa ikiwa ni sambamba na kutambulika kwenye mfumo.
Awali mwenyekiti wa wasafirishaji wa abiria kwa kutumia magari madogo (michomoko) ambaye pia ni katibu wa wamiliki wa magari hayo mkoani hapo Mussa Stephano amesema watazingatia maelekezo yote ya serikali katika kutekeleza shughuli zao.
Bonyeza maandishi haya yaliyokolezwa utazame yaliyosemwa na viongozi wa michomoko kwa video (bonyeza sentensi ya rangi ya bluu)
“Tutazingatia sheria inavyosema tunaenda kuyafuta yale yote ya nyuma doa lililotuchafua hatutaki lirudi tena tutazingatia kwenda mwendo unaotakiwa tofauti na ule wa awali,ubebaji wa abiria tutahakikisha wote wanakaa kwenye viti”amesema Stephano.
Julai 2022 alliyekuwa mkuu wa mkoa huu David Kafulila alipiga marufuku usafirshaji wa kutumia magari haya ( michomoko) baada ya kukiuka taratibu za kisheria.