skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Matinde Nestory, Mwanza

Maafisa wa Vyama vya Ushirika kutoka katika halmashauri za wilaya ya Magu, Ukerewe,Kwimba, Sengerema na Misungwi wamekabidhiwa pikipiki 6 kwa ajili ya kusaidia na kutekeleza usimamizi wa Vyama vya ushirika pamoja na kutoa huduma katika vyama vya Ushirika vilivyopo Mkoa wa Mwanza.

Akikabidhi pikipiki hizo leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katibu tawala msaidizi Mipango na uratibu Joachim Utaro ambaye amemkaimu Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Ngussa Samike amesema pikipiki hizo ambazo lengo ni Kusaidia katika  kutoa huduma kwa vyama vya ushirika,jamii na kuleta matokeo Chanya katika vyama vya Ushirika.

“Niwaombe maafisa Ushirika ambao mmepewa pikikipi hizi mzitunze mhakikishe mnazitumia kwa kuzingatia makusudi yaliyopangwa na serikali kufuata taratibu zote za utunzaji wa pikipiki hatutarajii kuona pikipiki hizi baada ya muda mfupi zimeharibika”amesema Utaro.

Ameongeza kuwa pikipiki zimetolewa Kutoa huduma kwa vyama vya Ushirika na jamii ambayo inahitaji msaada kwa masuala ya Ushirika katika utekelezaji wa majukumu ambayo yataongeza Chachu katika vyama vya Ushirika.

“Kwa yeyote yule ambaye atabadilisha matumizi hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake “amesema Utaro.

Nae mrajis msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Mwanza Lucas  Kiondere amesema pikipiki hizo zitasaidia maafisa Ushirika kuimarisha  usimamizi na udhibiti wa vyama vya Ushirika pamoja na kuweza kutatua changamoto kwa wakati.

“Kwa hizi halmashauri ambazo zimepatiwa pikipiki zilikuwa mwanzoni hazina vitendea kazi ambapo katika halmashauri tuna maafisa Ushirika 5 pikipiki 2 tumeangalia idadi ya vyama,idadi ya maafisa Ushirika waliopo kwenye halmashauri na uhitaji wa vitendea Kazi,pamoja na wingi wa vyama vya Ushirika katika halmashauri Zetu”amesema Kiondere.

Kwa upande wake Afisa Ushirika kutoka halmashauri ya Misungwi Cirily Kimaro amesema kupitia pikipiki hizi itasaidia kutatua changamoto ya umbali na kuvifikia vyama vya Ushirika maeneo ya pembezone kwa wakati.

“Tunashukuru Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na tume ya maendeleo ya Ushirika Tanzania kwa kutupatia pikipiki hizi ambazo zitaturahisishia kazi pamoja na kuimarisha vyama vya Ushirika”amesema Kimaro.

Hata hivyo Mkoa wa Mwanza una jumla ya vyama vya Ushirika 459 ambavyo vipo maeneo mbalimbali  katika halmashauri za mkoa wa Mwanza.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma