skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Maswa.

Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu limewakamata watu 7 kwa tuhuma za wizi wa vifaa mbalimbali vinavyohusika kwenye ujenzi wa reli ya kisasa eneo la Malampaka wilayani Maswa ikiwa ni pamoja  na lori la  kampuni ya (CCECC) ya  nchini China  inayojenga reli hiyo (SGR) 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Simiyu Blasius Chatanda amesema kufuatia operesheni kali wanayoifanya ya  kuwasaka wezi wanaohujumu ujenzi wa SGR ,wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakamata na baadhi kukimbia na kuacha vielelezo kama pikipiki  baiskeli

“Awamu ya kwanza tulikamata vitu vingi vikatolewa taarifa ya jumla lakini baada ya pale oparesheni ikaendelea katika mwendelezo wa oparesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 7 wamekamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo vyote vimeibiwa kwenye mradi huu (SGR) katika vitu vilivyoibiwa ni jumla ya lita 560 za mafuta aina ya diseli, pikipiki 8 ambazo zilikuwa zikitumika kubeba/kusafirisha mafuta hayo, mifuko 79 ya saruji, mipira 21 inayotumika kunyonyea, baiskeli 8, mabomba ya chuma 19, madumu tupu 20, wavu vipande 10, (nyanya ambazo zinatumika kwenye ujenzi wa karavati), nondo vipande vinne, vipande vitano vya red copper wire” amesema kamanda Chatanda na kuongeza kuwa:

Kamanda Chatanda anabainisha kuwa kumekuwepo na ongezeko la vitendo vya kuhujumu miradi ya maendeleo kitendo kinacholitia hasara na doa taifa hasa pale wakandarasi wa kigeni wanapokwamishwa kutekeleza wajibu wao wa kimkataba na kusababishiwa hasara.

Watu hawa walifika pahala wakadhani kuwa ni kitu cha kawaida kupora na kuhujumu miradi hii, waliiba mpaka gari yenye No  T 344  DXW aina ya howo  tani 12 lenye thamani ya sh milioni 180  ambalo lilikuwa likifanya kazi ya kusomba vifusi pamoja na mizigo mingine ndani ya mradi wa ujenzi  wa SGR” alisisitiza kamanda Chatanda

Lori hilo liliibiwa tarehe 27 /1/2023 ilipofika tarehe 29/1/2023 na lilikamatwa katika kijiji cha Mabama wilaya ya Urambo mkoani Tabora likiwa linasafirishwa kupelekwa kwa mteja ambaye mpaka sasa haikubainika jina lake na wapi alikuwa ingawa zipo fununu kuwa huenda ni mkoani Rukwa, Katavi au Mbeya.  

Kamanda Chatanda ameongeza kuwa Jeshi la polisi linatilia shaka kuwepo kwa mtandao wa wezi ndani ya kampuni za ujenzi kutokana na kwamba sii jambo rahisi kwa wizi wa gari kufanyika likiwa katika maegesho ya kampuni husika bila kuwepo na ushirikiano kati ya watu wan je na ndani ya kampuni yenyewe na kuahidi kufanya uchunguzi mkali utakaowezesha kukamatwa kwa wahusika.

“Watanznia wenzangu lazima tujenge uzalendo huu mradi ni wa kwetu wanufaika ni sisi kuendelea kuchelewa kwa mradi huu kutokana na wizi wa mali za mradi madhara yake ni makubwa tutaifanya serikali mwisho wa siku itumie fedha nyingi sana hela ambayo ingetumika kwenye miradi mingine” amesema kamanda Chatanda.  

 Siku za hivi karibuni makamanda wa jeshi la polisi kutoka mikoa mitatu ikiwemo Simiyu, Shinyanga na mwanza walitangaza kupambana na wanaohujumu mradi wa SGR kipande cha Isaka, Malampaka hadi Mwanza.

 

la polisi mkoa wa Simiyu limewakamata watu 7 kwa tuhuma za wizi wa vifaa mbalimbali vinavyohusika kwenye ujenzi wa reli ya kisasa eneo la Malampaka wilayani Maswa ikiwa ni pamoja  na lori la  kampuni ya (CCECC) ya  nchini China  inayojenga reli hiyo (SGR) 

Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Simiyu Blasius
Chatanda amesema kufuatia operesheni kali wanayoifanya ya  kuwasaka wezi
wanaohujumu ujenzi wa SGR ,wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakamata na baadhi
kukimbia na kuacha vielelezo kama pikipiki  baiskeli

“Awamu
ya kwanza tulikamata vitu vingi vikatolewa taarifa ya jumla lakini baada ya
pale oparesheni ikaendelea katika mwendelezo wa oparesheni hiyo jumla ya
watuhumiwa 7 wamekamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo vyote vimeibiwa
kwenye mradi huu (SGR) katika vitu vilivyoibiwa ni jumla ya lita 560 za mafuta
aina ya diseli, pikipiki 8 ambazo zilikuwa zikitumika kubeba/kusafirisha mafuta
hayo, mifuko 79 ya saruji, mipira 21 inayotumika kunyonyea, baiskeli 8, mabomba
ya chuma 19, madumu tupu 20, wavu vipande 10, (nyanya ambazo zinatumika kwenye
ujenzi wa karavati), nondo vipande vinne, vipande vitano vya red copper
wire” amesema kamanda Chatanda na kuongeza kuwa:

Kamanda
Chatanda anabainisha kuwa kumekuwepo na ongezeko la vitendo vya kuhujumu miradi
ya maendeleo kitendo kinacholitia hasara na doa taifa hasa pale wakandarasi wa
kigeni wanapokwamishwa kutekeleza wajibu wao wa kimkataba na kusababishiwa hasara.


Watu hawa walifika pahala wakadhani kuwa ni kitu cha kawaida kupora na kuhujumu
miradi hii, waliiba mpaka gari yenye No  T 344  DXW aina ya
howo  tani 12 lenye thamani ya sh milioni 180  ambalo lilikuwa
likifanya kazi ya kusomba vifusi pamoja na mizigo mingine ndani ya mradi wa
ujenzi  wa SGR” alisisitiza kamanda Chatanda

Lori
hilo liliibiwa tarehe 27 /1/2023 ilipofika tarehe 29/1/2023 na lilikamatwa
katika kijiji cha Mabama wilaya ya Urambo mkoani Tabora likiwa linasafirishwa
kupelekwa kwa mteja ambaye mpaka sasa haikubainika jina lake na wapi alikuwa
ingawa zipo fununu kuwa huenda ni mkoani Rukwa, Katavi au Mbeya.  

Kamanda
Chatanda ameongeza kuwa Jeshi la polisi linatilia shaka kuwepo kwa mtandao wa
wezi ndani ya kampuni za ujenzi kutokana na kwamba sii jambo rahisi kwa wizi wa
gari kufanyika likiwa katika maegesho ya kampuni husika bila kuwepo na
ushirikiano kati ya watu wan je na ndani ya kampuni yenyewe na kuahidi kufanya
uchunguzi mkali utakaowezesha kukamatwa kwa wahusika.

“Watanznia
wenzangu lazima tujenge uzalendo huu mradi ni wa kwetu wanufaika ni sisi
kuendelea kuchelewa kwa mradi huu kutokana na wizi wa mali za mradi madhara
yake ni makubwa tutaifanya serikali mwisho wa siku itumie fedha nyingi sana
hela ambayo ingetumika kwenye miradi mingine” amesema kamanda Chatanda.  

 Siku
za hivi karibuni makamanda wa jeshi la polisi kutoka mikoa mitatu ikiwemo
Simiyu, Shinyanga na mwanza walitangaza kupambana na wanaohujumu mradi wa SGR
kipande cha Isaka, Malampaka hadi Mwanza.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma