skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya wanahabari, vyombo vya Habari, taasisi za Habari na wamiliki kuhusu uwekaji wa mazingira rafiki ya upashanaji wa Habari nchini Tanzania hatimaye Serikali imekubali kukutana na wadau wote ili kujadiliana kuhusu furs ana changamoto za uhuru wa Habari nchini Tanzania

Kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla, kongamano hilo litafanyika kesho December 17 likiwakutanisha viongozi wa vyombo na taasisi za Habari, wahariri na wanafunzi wa vyuo vinavyofundisha taaluma ya uandishi wa Habari pamoja na wawakilishi wa serikali.

Bw. Abdulla amebainisha kuwa kongamano hilo pamoja na mambo mengine litajadili mada mbalimbali zitakazo wasilishwa na makundi mbalimbali kwa lengo la kuiwezesha Tanzania kuwa na mazigira bora na arafiki ya upashaji wa Habari.

Kwa habari zaidi tembelea ukurasa weyu wa twitter @fmbuha

Kwa takribani miaka mitano sasa tangu ilipotungwa na kupitishwa kwa sheria ya huduma za Habari ya mwaka 2016, waandishi wa Habari, taasisi na wahariri wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa vifungu kadhaa ambavyo si rafiki kwa tasnia hiyo mhimu katika jamii.

Miongoni mwa vikundi vilivyoanzishwa kwa ajili ya kusimamia majadiliano ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na sheria ana kanauni rafiki za Habari ni mtandao wa uhuru na haki ya kupata Habari iliyopewa jina la Coalition of Right to Information (CoRI) iliyoungwa na taasisi kadhaa ikiwemo TADIO, TEF, UTPC, MCT, MOAT, TAMWA, TWAWEZA na Jamii Forums

Wadau wa Kongamano hilo kutoka Dkt Rose Ruben kutoka TAMWA na Bw. Deusidedit Balile kutoka Jukwaa la wahariri TEF wanatoa hisia zao kuhusu umhimu na matarajio ya wanahabari katika kongamano hilo.

Viongozi kutoka CoRI wakielezea umhimu wa kongamano la wanahabari litakalofanyika December 17, 2022

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya Habari MAELEZO Bw. Rodney Mbuya akizungumza na Buha FM Radio amebainisha kuwa hatua mbalimbali za maandalizi ya kongamano hilo la kipekee zimekamilika na kwamba zimeudwa kamati mbalimbali za uratibu ikiwemo kamati ya Habari inayoundwa na wajumbe kadhaa wakiwemo Bw. Prosper Kwigize kutoka BUHA FM na Mtandao wa Radio jamii Tanzania, Nevile Meena kutoka Jukwaa la Wahariri, na Edwin Soko kutoka Klabu ya waandishi wa Habari ya mkoa wa Mwanza.

Kongamano hilo la aina yake litafanyika katika Ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma