skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  
Kituoo cha malezi na makuzi ya watoto wilayani Kasulu

Shirika la maendeleo la Korea KOICA kwa kushirikiana na UNESCO wamewezesha ujenzi wa vituo vya malezi na makuzi ya watoto katika mikoa ya Kigoma, Pemba, Mwanza, na Arusha kwa lengo la kuokoa kundi kubwa la watoto wanaopata matatizo ya kimalezi hususani ukatili, mimba na ajira katika umri mdogo

Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 228 umetekelezwa katika wilaya nne za Kasulu, Sengerema, Mkoani Pemba na Ngorongoro ambapo ni kata moja tu ambayo kutokana na ushawishi wa jamii ilichaguliwa kutekeleza mradi huo uliohusisha darasa la Watoto wadogo, jiko la kupikia chakula, zana za michezo na zana za kufundishia

Zaidi ya watoto 200 wenye umri wa kati ya miaka 2-4 watapatiwa huduma katika vituo hivyo kama sehemu ya malezi na maandalizi ya kuanza elimu ya awali.

Wilayani Kasulu mradi huo umetekelezwa katika Kijiji cha Titye katika jalmashauri ya wilaya ya Kasulu vijijini kwa thamani ya shilingi milioni 57.4 na inakadiriwa kuwa Watoto wapatao 30 hadi 50 wataandikishwa katika kipindi cha Januari 2022 kuanza kupata huduma malezi.

Akitoa maelezo ya mradi huo kabla ya kuukabidhi kwa uongozi wa serikali mkoani Kigoma, mwakilishi wa mkurugenzi wa UNESCOo Tanzania Bw. Kelvin Robert amebainisha kuwa uanzishwaji wa vituoo vya malezi na makuzi ya Watoto wadogo hususani wanaoishi katika mazingira magumu na waliotengwa na jamii ni suluhisho la makuzi na fursa ya elimu kwa Watoto wenyewe pamooja na wazazi wao

UNESCO imebainisha kuwa tafiti zinaonesha kuwa takribani asilimia 46 ya Watoto wanahitaji malezi maalumu kutokana na familia zao kutokuwa na utaaaratibu mzurii wa malezi, hasa katika vijiji ambavyo wazazi ni wakulima ambao hulazimika kuacha kaya zao kwa zaidi ya wiki moja wakihamia mashambani na kutelekeza Watoto wadogo wakilelewa na Watoto wenzao ambao pia hulazimika kuacha masomo ili kujihudumia.

Akipokea mradi huo kwa niaba ya serikali, kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw. …..ameishukuru Jamhuri ya watu wa Korea kwa kuufadhili mradi huo kupitia shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO na kukiri kuwa utasaidia kuleta mabadiliko ya kimalezi kwa jamii ya wilaya ya Kasulu.

Bw. Ameongeza kuwa, kutokuwepo na kituo cha malezi katika maeneo ya vijijini kunasababisha Watoto wengi kushindwa kujifunza wanapoanza elimu ya awali jambo linalopelekea walimu kupata kazi kubwa ya kuanza kuwapa Watoto malezi ya kijamii badala ya kuwafundisha kusoma na kuandika.

Kwa upande wake mwalimu Happy Mwakalinga wa shule ya msingi Nyankole katika Kijiji cha Titye ambako mradi huo umejengwa anataja kuwa changamoto ya Maisha ya kijijini huwagharimu Watoto wadogo hasa kwa kukosa malezi ya kifamilia, kijamii na kiafya hali inayopelekea udumavu hata wakati wa kijifunza darasani

Mwalimu Mwakalinga ametaja kuwa, shule za awali huwapokea Watoto wadogo wakiwa hawana ufahamu wowote w ahata namna ya kujisitiri, kuvaa, kucheza na wenzao, kula na Watoto wengine pamoja kutokuwa na stadi za usafi hali inayopelekea muda mwingi wa mwalimu kufanya kazi ya malezi ambayo ilistahili kuanzia kwa wazazi na katika vituo maalumu vya malezi ya Watoto maarufu kama kindergarten.

Viongozi wa kata ya Titye wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Bw. Elieza Moshi ameshukuru kwa eneo lao kuchaguliwa kuwa ya kwanza kujengewa kituo hicho na kuiomba serikali kushirikiana na wahisani kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kujenga uzio kwa ajili ya usalama wa Watoto na rasilimali za kituo.

Mwakilishi kutoka UNESCO Bw. Kelvin Robert amepokea ombi la Diwani na kuahidi kuwa watalifanyia kazii kwa kuhamasisha wadau wengine pia kujitokeza kukiendeleza kituo hicho.

Hicho ni kituo cha kwanza kujengwa na kumilikiwa na serikali mkoani Kigoma, vituo vingine vimejengwa na taasisi za kidini pamoja na watu binafsi ambao hutoza gharama kubwa kwa ajili ya malezi ya Watoto.  

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma