skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Idd Mashaka.

Afisa habari na Mawasiliano wa klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) Christina Mwagala ametoa taarifa ya Timu hiyo kujifua tayari kuwakabili wauaji wa Kusini Namungo FC Katika mchezo wa mzunguko wa tano (5) wa ligi kuu ya NBC utakaochezwa oktoba 01,2022 Uwanja wa Majaliwa Ruangwa mkoani Lindi.

 Akizungumza na waandishi wa habari Afifa huyo amesema “kama timu wanafahamu kuwa mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa wapinzani wao huku akijinasibu kwakusema kuwa wana kikoai cha VVIP  chenye uwezo wakupambana na kucheza soka safi na lakuvutia kwa manufaa ya Mashabiki wa KMC”.

“tunajua kwamba tunapoenda ugenini lazima mchezo utakuwa na ushindani na kama Timu ya KMC tumejidhatiti nakujipanga kikamilifu kuwa katika muendelezo mzuri katika michezo yetu kwakuzingatia michezo iliyopita” aliongeza Afisa huyo.

kwa upande mwingine Christina Mwagala amesema wiki iliyopita walikuwa na wakati mzuri wakufanya maandalizi tayari kwa mapambano nakuongeza kuwa mchezo huo wa oktoba moja utakuwa mchezo wao wanne kucheza ugenini, huku mchezo wa nyumbani ukiwa niule uliopita dhidi ya Ihefu FC ambao ulichezwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam nakumalizika kwa Wanakino Boys (KMC) kushinda magoli mawili kwa moja kabla ya kupisha michezo ya Kimataifa kwa mjibu wa kalenda ya FIFA.

KMC inajipanga kwa mchezo huo dhidi ya Namungo FC ikiwa tu ni baada ya kurejea kwa Ratiba ya michezo katika Ligi kuu ya NBC kwa mjibu wa Bodi ya Mpira wa Miguu Tanzania TPLB ambapo awali Ligi ilisimama kupisha Kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA jumaa lililopita.

Pia kwa upande mwingine baadhi ya Mashabiki wa Mpira miguu mkoani Morogoro wametoa maoni mseto kuhusu Timu hiyo ambayo inaonekana kuwa miongoni mwa timu bora nchini Tanzania kutokana na uwezo na ubora Nyota wa Timu hiyo huku wengi wao wakiisifu kwa kusema ni Timu bora na shindani.

Hata hivyo Timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mpaka sasa iko nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC ikiwa imeshacheza michezo minne pekee na kukusanya jumla Alama Tano(5)na magoli sita(6)yakufunga huku pia ikiwa imeruhusu magoli sita(6) .

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma