skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mchezo wa Mpira wa miguu ni mchezo wenye idadi kubwa ya mashabiki wenye mapenzi na mchezo huo ukilinganisha na michezo mingine inayochezwa katika nchi mbalimbali duniani.

Kutokana na mchezo huo kuwa na wapenzi wengi ndio maana ukawa na majina mengi sana, maana hutashangaa ukisikia soka, kandanda au Kabumbu, hayo ni mfano tu wa majina ya mchezo wa mpira wa miguu.

Katika Mkowa wa Kigoma mbali na kuwa na wapenzi wengi wa soka, pia mkoa huo umebarikiwa kuwa na wachezaji wengi, walioacha alama katika aifa hili kupitia mchezo huo, na wengine bado wanaendelea kulitumikia taifa.

Baadhi ya wachezaji wa zamani waliocheza katika timu mbalimbali za mpira wa miguu pamoja na timu ya Taifa wakitoka katika mkoa wa Kigoma ni pamoja na Alfonce Modesta, Nteze John, Edibily lunyamila, Selemani Matola, Said Suwed Scud, wilfredi kidau na wengine wengi.

Hata hivyo kipindi wakongwe hao wanancheza mpira, mchezo huo haukuwa kama ajira halisi ukilinganisha na sasa bali wengi walicheza mpira kama sehemu ya kujifurahisha tu na yenye ujira mdogo.

Kama ilivyo kwa Mkoa wa Kigoma, pia Mkoa wa Tanga umebarikiwa kuwa na wachezaji wa wengi wa soka ambao nao walicheza mpira na kupata majina makubwa japo hawakuwa na mafanikio kupitia soka.

Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Juma Mgunda, Ruben Mgaza, Hamphrey Mgaza na wengine wengi.  BUHA fm imepata bahati ya kuzungumza na Ruben Mgaza mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga pamoja na timu ya Taifa.

Katika mazungumzo na mchezaji huyo amepongeza shirikisho la soka nchini (TFF) kwa hatua kubwa ya kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

Moja ya jambo ambalo, amelizungumzia kwa hisia na masikitiko makubwa ni kwamba soka la Tanzania linaendeshwa kwa mtindo wa siasa, akitolea mfano uchaguzi mkuu wa Rais wa shirikisho la Soka Tanzania uliofanyika mwaka huu hapa nchini.

“inakuwaje uchaguzi unafanyika eti mgombea anapita bila ya kupingwa, hii haiwezekani wapo watu ambao ni wasomi walijitokeza kuwania nafasi lakini cha kushangaza majina yao yaliondolewa mapema, hii inauwa soka letu”, alisema mgaza.

Pia ameonesha kuhuzunishwa na namna makocha wazawa nchini Tanzania ambavyo hawapewi thamani sawa na ile thamani wanayopewa makocha wakigeni.

Amesema wapo makocha wenye uwezo mkubwa hapa nchini akimtaja freddy felix Minziro kuwa ni kocha mzuri lakini amekuwa akitumika kama daraja tu la kupandisha timu kutoka daraja la kwanza baada ya hapo ananyang’wanywa timu.

“hapa nchini wapo makocha wazawa ambao wanauwezo mkubwa sana katika kufundisha soka, lakini cha ajabu hawapewi heshima wanayostahili na badala yake wanapewa makocha wa kigeni, hii haitusaidii,” amesema Mgaza.

Mchezaji huyo wa zamani ya klab ya Yanga, amesema wachezaji wengi wa sasa hawajitumi kucheza kwa nguvu kama ilivyokuwa   katika wakati wao, japo kuwa wao walikuwa hawalipwi, na mchezo wa mpira ulikuwa kama sehemu ya kujitolea.

Muandaaji na msomaji wa Makala hii ni mimi Mussa Mkilanya, kwa maoni na ushauri tafadhali tembelea ukurasa wa Instagramna na facebook buha fm radio, na katika website www.buhafmradio.co.tz pia unaweza kutebelea ukurasa binafsi ‘mmkilanya’, au tuwasiliane kwa namba ya simu, 0652 213891.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma