skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Kama ilivyo sera ya Serikali kupitia wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kifungu 3(i) cha sheria ya wakala za serikali (Sura ya 245) iliyoanza kutumika mwaka 2000. Wakala ina jukumu la kukarabati na kuendeleza mtandao wa barabara kuu na barabara za mikoa Tanzania Bara.

Viongozi wa serikali kwa kushirikiana na wananchi wameendelea kushikamana katika kusimamia fedha za Serikali zinazofika kwenye maeneo yao ili kutumika kadiri ilivyokusudiwa na serikali kwenye kutengeneza na kuboresha miundombinu .

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Kirumbe Ng’enda ameiambia Buha habari kuwa  katika kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara  tayari Manispaa ya Kigoma ujiji  imeingia  kwenye mradi wa uboreshaji wa Miji na Manispaa ili kuboresha barabara zote Zenye urefu wa  kilometa 26.

Mradi huo utaanzia Kijiji cha Msimba kupitia Businde kwenda kichangachui,  kagera na kuunganisha daraja la mto luiche na nyingine itaanzia bangwe kupitia burega kwenda Posta Ujiji.

Mbunge Ng’enda wakati wa mahojiano na Buha hanari amesema wanahangaika kwa Sasa katika ujenzi mkubwa wa mradi wa barabara ambao uko katika Mpango wa jiji na Manisapaa.

Katika hatua nyingine Mbunge Ng’enda amesema Manispaa ya Kigoma Ujiji inaendelea kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa vyumba vya Madarasa ambapo umefikia asilimia 90 kwa baadhi ya Shule za Sekondari.

Nao baadhi ya Wananchi wa kata ya Bangwe ambao ni miongoni mwa kata zitakazonufaika na uboreshwaji wa barabara hizo, wamesema wamekuwa wakikumbana na changamoto kadhaa za kufanya shughuli za maendeleo kutokana na miundombinu ya barabara ya eneo Hilo kutokuwa   rafiki.

Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara nchi nzima ambapo mapema mwaka huu Meneja wa wakala wa barabara za Mjini na Vijijini TARURA, Manispaa ya Kigoma Ujiji  Mhandisi Issa Lyanga ameeleza kuwa mwaka huu wa fedha 2021-2022 Serikali imetoa shilingi Bilioni 3 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji  kwa ajili ya kuboresha na kujenga miundombinu ya barabara.

Imeandikwa na Emanuel Jonas

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma