skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu ameongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhamaji nguvu kazi, ukuzaji ujuzi kwa vijana, ukuzaji ajira na masuala mengineyo yanayohusu sekta ya kazi na ajira.

Akizungumza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema kuwa kikao hicho cha majadiliano kitafungua fursa kwa nchi hizo kushirikiana kwa karibu katika kubadilishana uzoefu juu ya  utekelezaji wa  majukumu sambamba na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko pamoja na watendaji walioambatana nao wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao hicho.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko amepongeza namna ambavyo Ofisi ya Waziri Mkuu katika kukuza fursa za ajira, viwango vya kazi sambamba na kusimamia usalama na afya kwa wafanyakazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Aidha, Ujumbe huo umetembelea ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja na Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA). 

Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko  anayesimamia masuala ya Kazi nchini Kenya. 

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma