skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Mwandishi Wetu Dodoma,

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka watendaji wa ofisi yake kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa malengo yanayopimika ili kuiwezesha serikali kufikia malengo na kuwahudumia wananchi.

Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo Septemba 5, 2023 mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Prof. Jamal Katundu ambae amehamishiwa Wizara ya Maji.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akikabidhiwa nyaraka kama ishara ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

Ameongeza kuwa, kazi ya kuhudumia wananchi haiwezi kufanikiwa ikiwa watumishi hawatashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kama timu huku wakizingatia weledi, uzalendo na ubunifu kwa maslahi mapana ya taifa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza menejimenti ya ofisi hiyo baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, hafla iliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Septemba 5, 2023.

Aidha, ameahidi kushirikiana na menejimenti na watumishi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ofisi hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Jamal Katundu ameishukuru Menenjimenti na Watumishi kwa ushirikiano waliompatia alipokuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ambao ulimwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma